Jumuiya Anglikana

(Elekezwa kutoka Ushirika wa Anglikana)


Jumuiya Anglikana (Anglican Communion) ni umoja wa makanisa yote yanayofuata mapokeo ya Kianglikana yaliyo na ushirika kamili na Kanisa la Uingereza.

Hakuna "Kanisa la Anglikana" lenye mamlaka duniani kote, kwa sababu kila kanisa la kitaifa au la kijimbo lina uhuru kamili. Pamoja na washiriki zaidi ya milioni mia moja na kumi, Jumuiya ya Anglikana ni dhehebu la Kikristo la tatu kwa ukubwa duniani, baada ya Kanisa Katoliki na Makanisa ya Kiorthodoksi.

Hali ya ushirika kamili inamaanisha kuwa ibada zote zinazofanywa katika kanisa moja zinatambuliwa na mengine. Baadhi ya makanisa hayo yanatumia jina "Anglikana", yakitambua uhusiano wa pekee na Kanisa la Uingereza; neno la Kilatini Anglicana linamaanisha "la Uingereza". Katika maeneo mengine Waanglikana wanatumia jina la "Kanisa la Kiaskofu" (Episkopali, Kiingereza: episcopalian).

Askofu Mkuu wa Canterbury aliye mkuu wa kidini wa Kanisa la Uingereza anatambuliwa kama ishara ya umoja huo. Hata hivyo hana mamlaka rasmi nje ya Uingereza yenyewe.

Ramani ya Dunia inayoonyesha majimbo ya Jumuiya Anglikana:
     Majimbo ya kitaifa      Kanisa la Kiaskofu la Marekani (Episcopal Church)      Kanisa la Jimbo la West Indies      Kanisa Anglikana katika Amerika ya Kati      Kanisa Anglikana ya Amerika ya Kusini      Kanisa Anglikana ya Afrika ya Kusini      Kanisa la Jimbo la Afrika ya Kati      Kanisa la Jimbo la Afrika ya Magharibi      Kanisa la Kiaskofu huko Yerusalemu na Mashariki ya Kati      Kanisa la Jimbo la Bahari ya Hindi      Lanisa Anglikana huko Aotearoa, New Zealand na Polynesia      Kanisa la Jimbo la Melanesia      Dayosisi ya Ulaya ya Kanisa la Uingereza      Makanisa nje ya jimbo chini ya Askofu Mkuu wa Canterbury      Kanisa la Jimbo la Asia Kusini Mashariki      Maeneo yasiyo na makanisa ya Kianglikana
Zingatia kwamba Kanisa la Eire linahudumia Eire ya Kaskazini (Northern Ireland) pamoja na Jamhuri ya Eire; Kanisa Anglikana la Korea linahudumia Korea Kusini na kinadharia (si hali halisi) pia Korea Kaskazini. Waanglikana wa Uhindi wamegawiwa kwa majimbo ya Kanisa la Uhindi Kaskazini na Kanisa la Uhindi Kusini. Dayosisi katika Ulaya (zamani Dayosisi ya Gibraltar katika Ulaya) ni sehemu ya jimbo la Canterbury likiwa pia na parokia katika Ureno na Hispania. Kanisa la Kiaskofu la Marekani lina parokia pia katika Ulaya.

Majimbo ya Ushirika wa Anglikana

hariri

Jumuiya hiyo inafanywa na majimbo yanayojitawala; kila jimbo lina dayosisi ndani yake zinazosimamiwa na askofu wake. Kuna pia maeneo kadhaa yasiyo na hadhi ya jimbo.

Kuna majimbo 38 ya Jumuiya Anglikana na kila moja linajitegemea na mkuu wake na katiba yake. Majimbo mara nyingi ni makanisa ya kitaifa (kama vile Tanzania, Kenya, Uganda, au Japani) au ya maeneo ya zaidi ya nchi moja (kama vile West Indies, Afrika ya Kati , au Asia ya Kusini-Mashariki).

 • Kanisa Anglikana huko Aotearoa, New Zealand, na Polynesia
 • Kanisa Anglikana la Australia
 • Kanisa la Bangladesh
 • Igreja Episcopal Anglicana do Brasil (Kanisa Anglikana la Kiaskofu la Brazil)
 • Kanisa Anglikana la Burundi
 • Kanisa Anglikana la Kanada
 • Kanisa la Jimbo la Afrika ya Kati
 • Kanisa Anglikana katika nchi za Amerika ya Kati
 • Jimbo la Kanisa Anglikana la Kongo
 • Kanisa la Uingereza lenye majimbo ya Canterbury na York
 • Kanisa Anglikana la Hong Kong (Kiaskofu)
 • Kanisa la Jimbo la Bahari ya Hindi
 • Kanisa la Ueire
 • Nippon Sei Ko Kai (Jumiya Anglikana huko Japani)
 • Kanisa la Kiaskofu huko Yerusalemu na Mashariki ya Kati
 • Kanisa Anglikana la Kenya
 • Kanisa Anglikana la Korea
 • Kanisa la Jimbo la Melanesia
 • Kanisa Anglikana la Meksiko
 • Kanisa la Jimbo la Myanmar (Burma)
 • Kanisa la Nigeria
 • Kanisa la India Kaskazini
 • Kanisa la Pakistan
 • Kanisa Anglikana la Papua Guinea Mpya
 • Kanisa la Kiaskofu la Ufilipino
 • Kanisa la Jimbo la Rwanda
 • Kanisa la Kiaskofu la Scotland
 • Kanisa la Jimbo la Asia ya Kusini Mashariki
 • Kanisa la India Kusini
 • Kanisa la Anglikana la Kusini mwa Afrika
 • Kanisa Anglikana la Amerika ya Kusini
 • Kanisa la Kiaskofu la Sudan
 • Kanisa Anglikana la Tanzania
 • Kanisa la Uganda
 • Kanisa la Kiaskofu huko Marikani
 • Kanisa huko Wales
 • Kanisa la Jimbo la Afrika ya Magharibi (Kamerun, Kabo Verde, Gambia, Ghana, Guinea, Liberia, Senegal, Sierra Leone)
 • Kanisa katika Jimbo la West Indies

Aidha, kuna makanisa sita yasiyo chini ya jimbo, na matano yapo chini ya mamlaka ya Askofu Mkuu wa Canterbury:

 • Kanisa Anglikana la Bermuda (chini ya Askofu Mkuu wa Canterbury)
 • Kanisa la Kiaskofu la Kuba (chini ya baraza lake)
 • Parokia ya Visiwa vya Falkland (chini ya Askofu Mkuu wa Canterbury)
 • Kanisa la Kiinjili la Kimitume la Kikatoliki la Lusitania katika Ureno (chini ya Askofu Mkuu wa Canterbury)
 • Kanisa la Kiaskofu la Matengenezo la Hispania (chini ya Askofu Mkuu wa Canterbury)
 • Kanisa la Ceylon ( Sri Lanka ) (chini ya Askofu Mkuu wa Canterbury)

Tazama pia

hariri

Tovuti za Nje

hariri