Usi (kwa Kiebrania ע֥וּץ uts, kwa Kigiriki Ως os, kwa Kiingereza Uz) ni jina la nchi linalotajwa katika Biblia ya Kiebrania na eneo alipoishi Ayubu. Pamoja na hayo kuna watu wanne wanaotajwa katika Biblia wenye jina la Usi.

Nchi ya Usi

hariri

Usi ni nchi alipoishi mhusika wa Biblia, Ayubu[1]. Nje ya kitabu cha Ayubu, nchi ya Usi imetajwa pia katika Yeremia 25:20 na katika Maombolezo 4:21.

Mahali kamili pa Usi hapajulikani. Wataalamu wa Biblia hujadili hasa sehemu mbili:

* Edomu ambayo ni eneo upande wa mashariki mwa kusini mwa bonde la mto Yordani

Mahali pa Usi si muhimu sana kwa kuelewa ujumbe wa Kitabu cha Ayubu .

Usi kama jina la binafsi

hariri

Usi mwana wa Aramu

hariri

Kufuatana na kitabu cha Mwanzo, Usi ni jina la binafsi na jina la ukoo pia. Katika Mwanzo 10:23 Usi ni mtoto wa kwanza wa Aramu na mjukuu wa Shemu. Ndugu zake waliitwa Huli, Getheri na Mashi. Usi iliendelea kutumiwa kama jina la kabila la Waaramu.

Mtaalamu Mwislamu Ibn Kathīr alimtaja Usi kama baba wa ʿAd ambaye ni chanzo cha kabila la ʿĀd linalotajwa katika Korani.

Usi mwana wa Nahori

hariri

Usi pia ni jina la mtoto wa kwanza wa Nahori ambaye alikuwa ndugu wa Abrahamu (Mwanzo 22:21). Mama yake aliitwa Milka na kaka zake walikuwa Buzi, Kemueli (baba wa Aramu), Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli (baba wa Rebeka aliyekuwa mke wa Isaka).

Usi mwana wa Dishan mki

hariri

Usi ni pia jina la mtoto wa kwanza wa Dishani, kiongozi wa Wahori (Mwanzo 36.28). Ndugu yake aliitwa Arani.

Usi baba wa Merari

hariri

Kuna pia Usi mmoja katika Kitabu cha Yuditi ambaye ni baba wa Merari na babu wa Yuditi aliye mhusika mkuu wa kitabu hicho (Yuditi 8:1).

Tanbihi

hariri
  1. Kitabu cha Ayubu 1.1

Viungo vya nje

hariri
  • Markus Witte: Uz . Katika: Michaela Bauks, Klaus Koenen (eds. Kamusi ya kisayansi ya Biblia kwenye mtandao (WiBiLex), Stuttgart 2006 ff