Vita ya Maji Maji

(Elekezwa kutoka Vita vya Majimaji)

Vita ya Maji Maji ulikuwa upingaji mkali wa Waafrika dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ujerumani katika maeneo ya kusini ya koloni la Afrika Mashariki ya Kijerumani.

Wilhelm Kuhnert, Mapigano huko Mahenge mwaka 1905.
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Vita hivyo vilishirikisha baadhi ya makabila ya kusini mwa Tanzania ya leo dhidi ya sera ya Kijerumani iliyoundwa kwa nguvu kuwalazimisha watu wa Tanganyika kulima zao la pamba.

Vita hivyo vilidumu kuanzia mwaka 1905 hadi 1907.

Chanzo kikubwa cha vita hii ni kwamba wanajamii walichoka kunyanyaswa na wakoloni. Baadhi ya manyanyaso hayo wakoloni waliwataka wanajamii kulima mazao ya kibiashara na walikatazwa kulima mazao ya chakula; kwa mantiki hiyo wanajamii walilima mazao ya biashara na kuacha kulima mazao ya chakula kwa lengo la kuwanufaisha wakoloni huku wao wakipata njaa kwa sababu ya kutolima mazao ya chakula kwa ajili ya kuwapatia chakula na huku adhabu kali ikitolewa kwa wale watakaopinga.

Kwa sababu hiyo wananchi walilazimika kufanya kazi huku wakilipwa mshahara mdogo au kutolipwa kabisa. Watu ambao hawakulazimika kufanya kazi ni watoto wadogo na wazee; kwa wale vijana wenye nguvu walifanyishwa kazi ngumu lakini kwa upande wa wasichana na mama wajawazito waliufanya kazi za ndani.

Moja ya changamoto walizozipata kwa upande wa vijana wa kiume ni kudhalilishwa kwa kupigwa mijeledi wakiwa uchi mbele ya wanawake wao na pia walitozwa pesa kubwa ukilinganisha na mshahara wanaopata ni kidogo: hizo ndizo baadhi ya changamoto walizozipata. Hivyo basi waliamua kukataa manyanyaso na masumbuko dhidi ya wakoloni.

Tunaona kwamba wahusika wakuu ni mtemi wa wanajamii Kinjekitile Ngwale na watemi wa Kijerumani.

Tunaona kwamba mtemi huyu wa kabila la Wangindo aliamini kwamba maji ndiyo silaha ya kipekee ambayo ingetumika kuwashinda wakoloni hata akawaambia wananchi wake kwamba wakoloni wakirusha silaha waseme "maji" kwa madai ya kuwa silaha itabadilika na kuwa maji.

Wanajamii wake waliamini kusikiliza, kwa hiyo basi vita ilipoanza wakoloni walipoanza kuwashambulia wanajamii walisema, "maji", lakini tunaona kwamba jinsi walivyokuwa wakisema "maji" ndivyo walivyozidi kushambuliwa.

Tunaona madhara makubwa waliyoyapata: ni wanajamii wengi walipoteza maisha kwa hiyo nguvukazi ilipungua kwa kiwango kikubwa, lakini tunaangalia chanzo kikubwa kabisa ni kupinga manyanyaso.

Marejeo

hariri
  • Pugu Hadi Peramiho - kimehaririwa na P. Gerold Rupper, OSB, BPNP, Peramiho 1988, ISBN 9967 67 031 1