Vitale wa Castronovo
Vitale wa Castronovo (Castronovo di Sicilia, Palermo, mwanzoni mwa karne ya 10 - Rapolla, Basilicata, 13 Oktoba 994) alikuwa mmonaki wa Ukristo wa Mashariki kwanza huko Agira, Sicilia, halafu sehemu mbalimbali ya Italia Kusini ya leo kufuatana na uvamizi wa Waarabu wa kisiwa hicho alipozaliwa, hadi alipofariki katika monasteri mojawapo kati ya zile alizozianzisha mwenyewe[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.