Wafiadini wa Korea

Wafiadini wa Korea ni kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.

Kati yao, 103 wametangazwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1]

Halafu, Paulo Yun Ji-Chung na wenzake 123 wametangazwa wenye heri na Papa Fransisko tarehe 16 Agosti 2014.

Pia kuna mipango ya kutangaza waliouawa na Wakomunisti wakati wa Vita vya Korea.[2]

MazingiraEdit

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[3] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[4].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Majina ya waliotangazwa watakatifuEdit

Majina ya waliotangazwa wenye heriEdit

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Korea and the church of martyrs. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-01-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-06.
  2. Bernie NiFhlatharta. Pressure on Pope to beatify Galway priest. Connacht Tribune – Galway City Tribune. Iliwekwa mnamo 24 September 2015.
  3. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
  4. The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.