Fransisko Choe Kyonghwan
Fransisko Choe Kyonghwan (Taraekkol, 1804 - Seoul, 12 Septemba 1839) alikuwa katekista wa Korea ambaye, kisha kupelekwa mbele ya liwali kwa imani ya Kikristo, hakukubali kuikana. Akiwa mfungwa gerezani na kuteswa kwa namna mbalimbali hakuacha kamwe sala na kazi ya katekesi hadi alipofikia kifodini[1].
Ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya dini yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Yeye[2] na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[3]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[4].
Mazingira
haririMwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[5] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[6].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/70020
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/70020
- ↑ "Korea and the church of martyrs". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-06.
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
- ↑ The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.
Marejeo
hariri- Attwater, Donald and Catherine Rachel John (1993). The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books. ISBN|0-14-051312-4.
- Dallet, Charles (1874). Histoire de l'Église de Corée, Volume 1. Paris: Librairie Victor Palmé.
- Dallet, Charles (1874). Histoire de l'Église de Corée, Volume 2. Paris: Librairie Victor Palmé.
- Fathers of the London Oratory (1859). The New Glories of the Catholic Church. London: Richardson and Son.
Viungo vya nje
hariri- Homily of Pope John Paul II given for the Mass for the canonization of the Korean martyrs
- List and brief description of martyrs
- History of the Missions Etrangeres de Paris MEP
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |