Andrea Kim Taegon

Sanamu ya Mt. Andrea Kim Taegon, padri Mkatoliki wa kwanza kutoka Korea.
Sanamu nyingine karibu na kanisa kuu la Myeongdong.

Andrea Kim Taegon (Hangul: 김대건 안드레아, Hanja: 金大建) (Solmoe, Dangjin, Korea, 1821Han River, Hanseong, Joseon, sasa Seoul, Korea Kusini, 1846), alikuwa padri wa kwanza wa Kanisa Katoliki mzaliwa wa Korea na ndiye msimamizi wa nchi.

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[1] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[2].

Wazazi wa Andrea waliongokea Ukristo na baadaye baba yake alifia dini hiyo kwa sababu ya kuacha dini yake ya awali.

Baada ya kubatizwa akiwa na umri wa miaka 15, Kim alisoma katika seminari ya Macau (China) na pia Lolomboy, Bocaue, Bulacan, Philippines.

Alipewa upadrisho huko Shanghai (1844) akarudi Korea ili kuinjilisha.

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Andrea Kim akawa mmoja kati ya maelfu waliouawa. Mwaka 1846, akiwa na miaka 25, aliteswa na hatimaye kukatwa kichwa karibu na Seoul kwenye Mto Han.

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri mwaka 1925, halafu tarehe 6 Mei 1984 Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wafiadini wengine 102 wa Korea, akiwemo Paulo Chong Hasang,

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 20 Septemba.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
  2. The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Andrea Kim Taegon kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.