Wafiadini wa Scilla

Wafiadini wa Scilla ni kundi la Wakristo 12 (wanaume 7 na wanawake 5) kutoka Scilla (leo Kasserine) waliouawa kwa ajili ya imani yao tarehe 17 Julai 180 huko Karthago, katika Tunisia ya leo.

Basilika la Wat. Yohane na Paulo mjini Roma, masalia ya wafiadini wa Scilla yanapotunzwa.

Majina[1] yao ni: Speratus, Nartzalus, Cintinus (Cittinus)[2], Veturius, Felix, Aquilinus,[3] Laetantius, Januaria, Generosa, Vestia, Donata[4] na Secunda.[5]

Masimulizi ya Matendo yao ni maandishi ya kwanza ya Kanisa la Afrika na mfano wa kwanza wa Kilatini cha Kikristo.

Sita kati yao walikuwa wameshahukumiwa. Kati ya waliobaki, wanaozungumziwa zaidi na Matendo hayo, Speratus alikuwa msemaji mkuu. [6]

Kisha kukiri imani yao, walitupwa gerezani kwa amri ya liwali Saturninus; kesho yake walipelekwa tena mahakamani wakiwa wamefungwa kwa pingu wakakiri tena kuwa Wakristo na kukataa kumuabudu Kaisari kama mungu. Hapo walihukumiwa wauawe, nao wote wakapiga magoti na kumshukuru Mungu huku wakikatwa vichwa kwa upanga[7].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.[8]

Sikukuu yao huadhimishwa siku ya kifodini chao[9][10].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Two of these bear Punic names (Nartzalus, Cintinus), but the rest are Latin names.
  2. https://dacb.org/stories/tunisia/cittinus/
  3. Smith, Clyde Curry (2004). "Dictionary of African Christian Biography". Dictionary of African Christian Biography. http://www.dacb.org/stories/tunisia/aquilinus.html. Retrieved 22 April 2017.
  4. https://dacb.org/stories/tunisia/donata/
  5. "Church Fathers: The Passion of the Scillitan Martyrs". Newadvent.org. Iliwekwa mnamo 2013-07-17.
  6. He claimed for himself and his companions that they had lived a quiet and moral life, paying their dues and doing no wrong to their neighbors. But when called upon to swear by the name of the emperor, he replied "I recognize not the empire of this world; but rather do I serve that God whom no man hath seen, nor with these eyes can see." The response was a reference to the language of 1 Tim 6:16. In reply to the question, "What are the things in your satchel?", he said "Books and letters of Paul, a just man." The martyrs were offered a delay of 30 days to reconsider their decision, which they all refused.
  7. https://www.santiebeati.it/dettaglio/63120
  8. "Scillitan Martyrs, in North Africa", Antiochian Orthodox Christian Archdiocese
  9. Martyrologium Romanum
  10. https://catholicsaints.info/martyrs-of-scillium/

Marejeo

hariri
  • Stokes, G.T., "Scillitan Martyrs", Dictionary of Christian Biography, (Henry Wace ed.), John Murray, London, 1911
  • H. Musurillo, trans., "The Acts of the Scillitan Martyrs" in The Acts of the Christian Martyrs (Oxford: University Press, 1972).

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.