Wilaya ya Biharamulo
Wilaya ya Biharamulo ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Kagera, Tanzania kaskazini magharibi, yenye postikodi namba 35600 [1].
Wakazi
haririKatika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 323,486 [2] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 457,114 [3].
Wasubi, walio kundi linalohesabiwa kati ya Wanyambo, Wazinza, Wahaya na Walongo, ndio wakazi asilia wa wilaya ya Biharamulo,
Jina
haririInasemekana, asili ya jina Biharamulo ni neno la Kisubi "Niharemuno" likimaanisha "Ni mbali mno". Neno hilo lilikuwa jibu la mzee mmoja kwa Mzungu aliyemuuliza wakati wanasafiri pamoja kutoka Geita kwenda kijiji cha Nyarubungo kilichopo Biharamulo. Mzungu alimuuliza Mzee huyo, "How many kilometers from here to Nyarubungo?" yaani, "Kuna kilomita ngapi kutoka hapa kwenda Nyarubungo?" na mzee yule alijibu, "niharemuno" akimaanisha "ni mbali mno'.
Historia
haririWilaya hii pamoja na Wilaya ya Karagwe zilianzishwa na kutangazwa rasmi na Gavana wa Kiingereza Richard Turnbull mwaka 1958.
Shughuli
haririUchumi ni pamoja na ufugaji wa ng'ombe na mbuzi, kilimo cha kahawa, migomba, mihogo, mahindi, maharage na zao la pamba katika maeneo machache. Shughuli nyingine za kiuchumi katika wilaya ya Biharamulo ni uvuvi, biashara na uchimbaji madini.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ Sensa ya 2012, Kagera - Biharamulo-District-Council
- ↑ https://www.nbs.go.tz
Viungo vya nje
hariri- About maternal & newborn health (MNH) in Biharamulo District Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Tovuti ya BOSEDA Biharamulo originating socio - economic development association Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Biharamulo - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ||
---|---|---|
Biharamulo Mjini | Bisibo | Kabindi | Kalenge | Kaniha | Katahoka | Lusahunga | Nemba | Nyabusozi | Nyakahura | Nyamahanga | Nyamigogo | Nyantakara | Nyanza | Nyarubungo | Runazi | Ruziba |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Biharamulo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |