Wanyambo ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Karagwe. Watu wake ni wakulima na wafugaji.[1]

Lugha yao ni Kinyambo ambacho kinashabihana na Kinyankole, Kilongo na Kihaya.

Wengi huwachanganya Wanyambo na Wahaya kwa kuwa lugha zao zinafanana. Inasemekana kwamba hata Wanyambo wenyewe, hasa waishio nje ya Karagwe, hawana ufahamu kama wao ni Wanyambo au ni Wahaya.

Kuhusu Wanyambo wanasema walitokana na kizazi cha Kanyambo mtoto wa Ruhanga ambaye alitumwa kuanzisha nchi ya Karagwe toka Bunyoro, lakini watu husema kuwa nchini Uganda kuna mababu zao waliozaliwa kutoka Karagwe na zipo aina ya ndizi asilia inaitwa enyambo, na wapo ng'ombe asilia wenye pembe fupi waitwaye Ente ye Nyambo.

Wanyambo ni kabila lililokuwa miongoni mwa makabila makubwa na yenye nguvu za kivita na kiuchumi. Watu wa kabila hili la wanyambo walikuwa na ufalme ulioongozwa na wafalme Abakama 14 kwa nyakati tofauti.

Kwa sasa baadhi ya Wanyambo wamechanganyikana na asili ya Kinyarwanda kwa sababu wakimbizi waliishi Karagwe na kuoana au kuzaliana na wenyeji wao.

Wanyambo wana utamaduni tofauti na makabila mengine ya mkoa wa Kagera. Kwa mfano, mavazi yaliyotumika (yalifahamika kama "embugu") zilitokana na magome ya miti iitwayo kwa Kinyambo "emitoma".

Wametawaliwa na viongozi walioitwa "omukama" na walio maarufu sana mpaka sasa ni: omukama Rumanyika na omukama Ruhinda Snr (balozi mstaafu) anayekaa makao makuu huko Karagwe, Nyakahanga. Watu wengine wajulikanao ni familia ya Gabagambi walioishi Nyakahanga karibu na kiongozi huyo wa jadi.

Wanyambo hupenda kula ndizi kama chakula chao. Zamani ungemuuliza Mnyambo halisi alichokula, angesema "nalya ebitoke", maana "nimekula chakula", ila kama angekula ugali angesema "tinalya akantu", maana "sijala chochote".

Wilaya ya Karagwe hariri

Magharibi ya ziwa Victoria ipo wilaya ya Karagwe na makao makuu ya wilaya hii ni Kayanga. Mji huo ni wa zamani na ilijulikana sana ndani na nje ya Tanzania. Uliongozwa sana na Mtemi (Omukama) Rumanyika aliyekuwa na himaya yake huko Bushangaro Bweranyange.

Karagwe inapakana na wilaya za Biharamulo, Missenyi na Ngara na inapakana na nchi za Rwanda na Uganda, japo kwa sasa imezaa wilaya mpya ya Kyerwa ambayo inazo koo nyingi kutoka maeneo mbalimbali hasa Buganda (Toro na Kochi) mfano Abatundu, Abazigaba, n.k. Viongozi katika koo hizo waliitwa Abategeki/Omutejechi. Baadhi ya koo hizo ni Zilimu, Mtehimbwa ambazo zilikuwa za Watejechi na mpaka sasa zipo maeneo ya Nyakatuntu huko Kyerwa.

Karagwe inakaliwa na kabila la Wanyambo (Abhanyambo) wanaozungumza lugha yao ya Kinyambo (Orunyambo) japo kwa sasa kuna mchanganyiko wa makabila mengi na wageni wengi. Jina Karagwe inasemekana na simulizi za wazee mbalimbali na watafiti wa historia ya Karagwe, kwamba linatokana na kilima (ziwa Kitete) kinachopatikana kusini magharibi mwa makao makuu ya wilaya hii, kijiji cha Kandegesho Kwa Omukama (nono ya malija yaani ukoo wa abhasita).

Karagwe ni eneo la kihistoria ya Tanzania ya kaskazini magharibi, upande wa magharibi wa Ziwa Viktoria Nyanza, karibu na mpaka wa Burundi. Sehemu kubwa ya eneo hili leo ni wilaya ya Karagwe katika Mkoa wa Kagera.

Karagwe ya leo imetoka mbali na kila kizazi kinachozuka kinaongeza yake juu ya Karagwe na wao wenyewe.

Watawala wa Karagwe hariri

Watawala wa Karagwe walikuwa na cheo cha "Umugabe". Nasaba ilianzishwa mnamo mwaka 1450 na mtemi Ruhinda I aliyeitwa pia Bunyambo.

1675 - 1700 Ruhinda V

1700 - 1725 Rusatira

1725 - 1750 Mehinga

1750 - 1775 Kalemera I Ntagara Bwiragenda (alifariki 1775)

1775 - 1795 Ntare V "Kiitabanyoro"

1795 - 1820 Ruhinda VI Orushongo "Lwanyabugondo" (b. 1777 - d. 1820)

1820 - 1853 Ndagara I "Luzingamcucu lwa nkwanzi"

1853 - 1881 Rumanyika I Rugundu

1882 - 1886 Ndagara II Nyamkuba

1886 - 1893 Kalemera II Kanyenje

1886 - 1893 Kakoko -Regent

1893 - 1914 Ntare VI

1914 - 1916 Kahigi -Regent

1916 - 1939 Daudi Rumanyika II

1939 - 1962 - 9.12. B. Itogo Ruhinda VII

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanyambo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.