Yakobo Israeli

katika Mwanzo, mwana wa Isaka, anayejulikana pia kama Israeli; babu wa Waisraeli
(Elekezwa kutoka Yakobo-Israeli)

Yakobo au Israeli (kwa Kiebrania Yaʿaqov au Ya'ãqōb, kwa Kigiriki ᾿Ιακώβ, kwa Kilatini Iacob, kwa Kiarabu Yaʿqūb) katika Biblia ni mwana mdogo wa Isaka na Rebeka, hivyo ni mjukuu wa Abrahamu na Sara.

Mchoro wa Tiepolo (1726-1728): Raheli na sanamu alizoziiba (sehemu inahomhusu Yakobo), huko Udine (Italia).
Mchoro wa Gustavo Doré: Mapambano ya Yakobo na Malaika (1855)

Ndiye aliyezaa watoto wa kiume 12 ambao ndio mababu wa makabila 12 ya taifa la Israeli.

Habari zake zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Desemba[1].

Katika Biblia

hariri

Kadiri ya Mwa 25:19-34, Rebeka alimzalia Isaka watoto pacha wenye sura na silika tofauti, Esau na Yakobo. Wa kwanza analaumiwa hasa kwa kupuuzia baraka ya Mungu iliyokuwa haki ya kifunguamimba: kwa sahani ya dengu alikubali kukosa neema zile zote alizojitwalia Yakobo kwa imani yake (Eb 12:16-17).

Mwa 27 inasimulia jinsi Yakobo, akifundishwa na mama yake, alivyoweza kubarikiwa na baba. Ingawa uongo wake haukubaliki (Hos 12:3-5), Mungu alithibitisha baraka ya Isaka kadiri ya desturi yake ya kumpendelea mdogo: hivyo Yakobo, aliyekimbia nchi yake ana fimbo tu, alirudi miaka ishirini baadaye ana wake 4, watoto 11 na mifugo wengi ajabu (Mwa 32).

Kabla hajaingia nchi yake Mungu alishindana naye usiku kucha akalazimika kumbariki na kumtajia jina jipya, Israeli.

Baada ya kuishi katika nchi ya Kanaani, alimalizia maisha yake Misri alipohamia pamoja na wazao wake wote kutokana na njaa. Hata hivyo alidai akazikwe kwao, karibu na wazee wake, katika nchi aliyoahidiwa na Mungu kuwa itamilikiwa na wajukuu wake.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yakobo Israeli kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.