4°40′07″S 39°11′35″E / 4.668654°S 39.193150°E / -4.668654; 39.193150
Yasini (zamani pia Jassin, Jassini[1]) ni kijiji cha kata ya Mayomboni, Mkoa wa Tanga, Tanzania. Kijiji hiki kipo kwenye mpaka kati ya Tanzania na Kenya, karibu na mwambao wa Bahari Hindi kwenye pande zote mbili za mpaka.

Wakati wa ukoloni kulikuwa na kituo cha forodha na polisi lakini tangu kujengwa kwa barabara barani ndani zaidi hakuna kituo tena.

Eneo la mapigano ya "Jassini", lilivyochorwa na Lettow Vorbeck.

Mapigano ya Yasini - Jassini

hariri

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kulikuweko mapigano kwenye Januari 2015. Mwisho wa mwaka 1914, baada ya mapigano ya Tanga, vikosi 3 vya jeshi la Kihindi-Kiingereza kutoka Mombasa vilivuka mpaka na kuvamia Yasini. Mnamo tarehe 18-19 Januari [2] kiongozi Mjerumani Paul von Lettow-Vorbeck alishambulia vikosi hivyo. Alitegemea ya kwamba Waingereza wangeleta askari zaidi kutoka Mombasa mara wakisikia kuhusu shambulio lake, akaficha vikosi kadhaa vya Schutztruppe porini na kuwasubiri Waingereza. Vikosi vya Wahindi walipaswa kusalimisha amri baada ya kujitetea kwa siku 1 kwa sababu walishindwa kupata maji ya kunywa. Wakati huohuo vikosi vingine vya askari 3000 vilifika kutoka Mombasa vikashambuliwa ghafla na askari wa Schutztruppe 1000. Jioni ya tarehe 19 Januari Waingereza waliondoka wakarudi Mombasa baada ya kupotewa na zaidi ya wanajeshi 700.

Lettow Vorbeck aliandika baadaye ya kwamba ushindi haukuweza kumfurahisha kwa sababu hata upande wake vifo vilitokea pamoja na kwisha kwa risasi. Aliamua kuepukana na mapigano makubwa kwa sababu alijua Waingereza wangeweza kuongeza wanajeshi tena na tena ilhali yeye alikuwa tu na idadi hiyohiyo asingeweza kupoteza maafisa na askari tena jinsi ilivyotokea Yasini. Hapo aliamua kuendelea kwa mitindo ya vita ya msituni.

Marejeo

hariri
  1. Katika orodha ya Misimbo ya Posta (Tanzania Post Code list) jina laandikwa "Jasini" - iliangaliwa Juni 2018
  2. K.K Adgie, Askaris, Asymmetry, And Small Wars: Operational Art And The German East African Campaign, 1914-1918, uk

Kujisomea

hariri