Yohane Antoni Farina

Yohane Antoni Farina (11 Januari 18034 Machi 1888) alikuwa askofu mmojawapo wa Kanisa Katoliki nchini Italia, kwanza Treviso halafu Vicenza, na mwanzilishi wa shirika la Masista Walimu wa Mt. Dorotea Mabinti wa Mioyo Mitakatifu.

Picha yake halisi.

Alisifiwa kwa uchungaji wake, kwa ukarimu wake kwa maskini wa aina zote na kwa kuinua vijana kwa malezi.[1]

Ndiye aliyempa upadrisho atakayekuwa Papa Pius X[2].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 4 Novemba 2001 na Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 23 Novemba 2014.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.