Yohane wa Nepomuk
Yohane wa Nepomuk (kwa Kicheki: Jan Nepomucký; kwa Kijerumani: Johannes Nepomuk; kwa Kilatini: Ioannes Nepomucenus[1]; Nepomuk, 1345 hivi – Prague, 20 Machi 1393[2]) alikuwa padri wa Bohemia (leo nchini Ucheki). Aliuawa kwa kutoswa mtoni Vltava kutoka darajani kwa agizo la mfalme Wenseslaus IV, mfalme wa Warumi na wa Bohemia.
Baadaye ilisimuliwa kwamba alikuwa muungamishi wa malkia na kwamba alikataa ombi la mfalme la kutoboa siri za kitubio. Kwa msingi huo anahesabiwa kama mfiadini wa kwanza wa siri ya kitubio na msimamizi dhidi ya masingizio.[2]
Alitangazwa mwenye heri tarehe 31 Mei 1721, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 19 Machi 1729.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 20 Machi[3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Sanctus Johannes Nepomucenus Christi Heiliger Blut-Zeug. 1723.
- ↑ 2.0 2.1 Krčmář, Mgr. Luděk. "Saint John of Nepomuk". SJN.cz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-02-21.
If in 1369 John of Pomuk was a notary public, he must have been more than twenty years old. Thus he was probably born sometimes between 1340 and 1350 [1349].
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
hariri- The "official" page of John of Nepomuk Ilihifadhiwa 11 Oktoba 2004 kwenye Wayback Machine.
- Catholic Encyclopedia (1910): "St. John Nepomucene" This provides a Catholic point of view
- Christian Classics Ethereal Library at Calvin College: "John of Nepomuk" This provides a Protestant point of view. It was also the source of the initial version of this article.
- Zdarns.cz Ilihifadhiwa 6 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- St. John Nepomuk, Martyr at the Christian Iconography web site
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |