Waraka wa pili wa Yohane

(Elekezwa kutoka 2Yoh)
Agano Jipya

Waraka wa pili wa Yohane ni kitabu kifupi kuliko vyote 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi

hariri

Kuanzia karne ya 5 mapokeo yamemtaja Mtume Yohane kuwa mwandishi wa barua hii, kwa sababu yaliyomo, misamiati na mtindo wa mawazo vinalingana na vile vya Waraka wa kwanza wa Yohane. Lakini barua yenyewe inamtaja tu "mzee" kuwa mwandishi wake.

Mahali na muda wa uandishi

hariri

Sawa na maandishi mengine ya jumuia za Yohane, barua hiyo inafikiriwa kuandikwa mwishoni mwa karne ya 1 huko Efeso ili kuangalisha dhidi ya wazushi. Katika barua hii linaonekana kwa mara ya kwanza jina la "Mpingakristo".

Walengwa

hariri

Walengwa ni Wakristo wa Kanisa linaloitwa "Bibi mteule".

Marejeo

hariri
  • Robert Dabney, "The Doctrinal Various Readings of the New Testament Greek", 1894: p. 32.

Kiungo cha nje

hariri
  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili
  Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa pili wa Yohane kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.