Adalbert wa Prague

Adalbert wa Prague (kwa Kicheki Vojtěch, kwa Kipolandi Wojciech, kwa Kijerumani Adalbert, jina alilojichagulia alipopewa Kipaimara na Adalbert wa Magdeburg ; Libice, leo nchini Ucheki 956 hivi – Tenkitten, leo nchini Urusi, 23 Aprili 997) alikuwa askofu wa Prague (Ucheki) tangu mwaka 983.

Mt. Adalbert wa Prague.
Fuvu la kichwa chake.
Masalia katika sanduku la fedha katika kanisa kuu, Gniezno, Poland.

Huko alipatwa na matatizo mengi akafanya safari nyingi kwa jina la Kristo, akijitahidi kwa nguvu zote kung'oa desturi za Kipagani. Alipotambua kwamba matunda yake ni machache, alikwenda Roma akawa mmonaki Mbenedikto.

Hatimaye alikwenda Polandi ili kuwaletea imani Waprusia, akachomwa kwa mikuki na Wapagani kadhaa[1].

Mwaka 999 alitangazwa na Papa Silvesta II kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 23 Aprili[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.