Albin Ekdal
Albin Ekdal (alizaliwa 28 Julai 1989) ni mshambuliaji wa Uswidi ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya Sampdoria iliyopo Serie A ya Italia.
Jinsia | mume |
---|---|
Nchi ya uraia | Uswidi |
Nchi anayoitumikia | Uswidi |
Jina halisi | Albin |
Jina la familia | Ekdal |
Tarehe ya kuzaliwa | 28 Julai 1989 |
Mahali alipozaliwa | Stockholm |
Baba | Lennart Ekdal |
Ndugu | Hjalmar Ekdal |
Kazi | association football player |
Nafasi anayocheza kwenye timu | Kiungo |
Muda wa kazi | 2007 |
Medical condition | COVID-19 |
Mchezo | mpira wa miguu |
Namba ya Mchezaji | 8 |
Ameshiriki | Kombe la Dunia la FIFA 2018, UEFA Euro 2016 |
Ligi | Bundesliga |
Kazi ya klabu
haririBrommapojkarna
haririAlbin Ekdal alianza kazi yake ya kucheza akiwa na klabu ya Brommapojkarna mwanzoni mwa msimu wa 2007 Allsvenskan. Alicheza hasa kama kiungo mkabaji lakini pia kama kiungo mshambuliaji.
Juventus
haririMnamo tarehe 23 Mei 2008, alisaini mkataba wa miaka minne na klabu Juventus F.C .. Ekdal alikata kusaini katika klabu nyingine, ikiwa ni pamoja na Chelsea na Inter, kabla ya kusaini makataba na klabu ya Juventus FC. Ekdal alicheza Serie A kwa maraya kwanza mnamo 18 Oktoba 2008 katika mechi ambayo walifungwa 1-2 dhidi ya klabu ya Napoli wakati aliingia kama mchezaji wa akiba dakika ya 75, akichukua nafasi ya Christian Poulsen.
Siena
haririMnamo tarehe 15 Julai 2009, A.C. Siena walimsaini Ekdal kwa mkopo kutoka katika klabu ya Juventus F.C. alcheza mechi 27.
Bologna
haririTarehe 28 Juni 2010, Juventus F.C. waliuza 50% ya hisa zao Ekdal katika klabu ya Bologna.
Cagliari Calcio
haririTarehe 21 Agosti 2011 aliuzwa katika mpango wa ushirikiano na klabu ya Serie A wenzake Cagliari Calcio. Mnamo tarehe 28 Septemba 2014, Ekdal alifunga goli lake la kwzanza katika klabu ya Cagliari baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Inter Milan.
Hamburger SV
haririMnamo tarehe 18 Julai 2015,alisajiliwa katika klabu ya Ujerumani itwayo Hamburger SV alisaini kutoka katika klabu ya Cagliari kwenye mpango wa miaka minne(4) kwa pauni 4.5 milioni a.Alipewa jezi ya namba 20. Tarehe 3 Machi 2017, Ekdal alifunga goli lake la kwanza katika ligi ya Bundesliga katika ushindi wa 1-0 dhidi ya klabu yaHertha BSC.
Sampdoria
haririMnamo 14 Agosti 2018, baada ya miaka mitatu (3) akiwa na klabu ya Hamburger SV, Ekdal alirudi tena Serie A kwa kusaini mkataba katika klabu ya Sampdoria.
Kazi ya kimataifa
haririEkdal alicheza kwa mara ya kwanza katika Timu ya taifa ya Uswidi mnamo 10 Agosti 2011 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ukraine.Mnamo Mei 2018 alitajwa katika kikosi cha watu 23 kwa ajili ya kuiwakilisha nchi ya Uswidi katika Kombe la Dunia la FIFA 2018 nchini Urusi.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Albin Ekdal kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |