Anthony Petro Mayala

(Elekezwa kutoka Anthony Petro Mayalla)

Anthony Petro Mayala (Aprili 23, 1940Agosti 19, 2009) alikuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Tanzania. Alisimikwa rasmi tangu Februari 28, 1988, [1] akaendelea hadi kifo chake mnamo 2009.

Mayala alikuwa mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Saint Augustine cha Tanzania (SAUT) na wa Kituo cha Matibabu cha Weil Bugando (WBMC).

Maisha ya Awali

hariri

Anthony Petro Mayala alizaliwa katika kijiji cha Nyamhungu (Nera), Parokia ya Ng'wabagole ya Wilaya ya Kwimba, Tanganyika (Tanzania hivi sasa) mnamo Aprili 23, 1940. [1] Alisoma shule ya msingi na sekondari katika Wilaya ya Kwimba. Mayala alisoma katika Chuo Kikuu cha Loyola Chicago kutoka mwaka 1973 hadi 1975, ambapo alipata digrii katika masuala ya elimu.

Mayala alipata daraja ya Upadri mnamo Desemba 20, 1970, katika Parokia ya Ibindo, Jimbo la Mwanza. [1] Aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma mnamo Februari 22, 1979.

Aliwahi kuwa Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuanzia Juni 1983. [1]

Mayala alisimikwa rasmi kama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza mnamo Februari 28, 1988. [1] Aliendelea kuwa Askofu Mkuu hadi kifo chake mnamo 2009.

Anthony Petro Mayala aliugua ghafla takriban saa 10:00 asubuhi mnamo Agosti 19, 2009, na kukimbizwa hospitalini. [1] Mayalla alifariki kutokana na mshtuko wa moyo katika Kituo cha Matibabu cha Weil Bugando katika Jiji la Mwanza, Tanzania, takriban saa 2:30 usiku mnamo Agosti 19, 2009. Alikuwa na umri wa miaka 69.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 Magubira, Patty. "Catholic cleric Mayalla dies of heart attack", The Citizen (Tanzania), 2009-08-20. Retrieved on 2009-08-20. Archived from the original on 2010-01-05.  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "citizen" defined multiple times with different content

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.