Jimbo Katoliki la Musoma
Jimbo Katoliki la Musoma (kwa Kilatini "Dioecesis Musomensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Eneo lake ni la kilometa mraba 25,150 (Mkoa wa Mara isipokuwa wilaya ya Bunda na parokia mbili katika wilaya ya Musoma vijijini) na lina wakazi 1,040,000, ambao kati yao Wakatoliki ni 215,000 (20.7 %). Parokia ziko 30.
Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Mwanza.
Askofu wake ni Michael George Mabuga Msonganzila na makao yake ni Musoma mjini. Kanisa kuu limejengwa kwa heshima ya Mtume Paulo.
Anasaidiwa na mapadri 58, ambao kati yao 38 ni wanajimbo na 20 ni watawa. Kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 3,707. Pia kuna mabruda 12 na masista 200.
Historia
hariri- 11 Aprili 1946 kuanzishwa kama apostolic vicariate kwa hati Quo in Tanganikensi ya Papa Pius XII.
- 24 Juni 1950 kugawanyika kati ya Maswa (leo Jimbo Katoliki la Shinyanga) na Musoma.
- 5 Julai 1957 kuanzishwa kama dayosisi kwa hati Quam pollicitationem ya Papa Pius XII.
- 27 Novemba 2010: Kuanzishwa kwa Jimbo jipya la Bunda kutokana na jimbo la Musoma na jimbo kuu la Mwanza .
Uongozi
hariri- Joseph Blomjous, M.Afr. (11 Aprili 1946 - 25 Juni 1950 alipokabidhiwa Jimbo Kuu la Mwanza)
- Giuseppe Gerardo Grondin, M.M. (1950 - 1957 alipofariki)
- John James Rudin, M.M. † (5 Julai 1957 - 12 Januari 1979 alipojiuzulu)
- Anthony Mayala † (12 Januari 1979 - 18 Novemba 1987 alipofanywa askofu mkuu wa Mwanza)
- Justin Tetmu Samba † (25 Oktoba 1988 - 23 Agosti 2006 alipofariki)
- Michael George Mabuga Msonganzila, kuanzia tarehe 10 Novemba 2007
Viungo vya nje
hariri- [1]
- [2] Archived 14 Julai 2014 at the Wayback Machine. sul Sito della Conferenza episcopale della Tanzania
- Hati Quo in Tanganikensi, AAS 39 (1947), uk. 76
- Hati Quam pollicitationem, AAS 50 (1958), uk. 137
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Musoma kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |