Kiribati ni nchi ya visiwani ya Polynesia na Mikronesia katika Pasifiki karibu na ikweta yenye wakazi 100,000 hivi.

Kiribati

Eneo lake ni visiwa 33 vilivyosambaa kwa 5,200,000 km². Visiwa 32 vimepangwa katika vikundi vinne:

Mji mkuu wa Bairiki uko kwenye kisiwa cha Tarawa.

Ramani ya Kiribati

Jiografia hariri

Kiribati ina eneo pana sana; umbali kati ya kisiwa cha magharibi kabisa cha Banaba hadi kisiwa cha mashariki kabisa cha Millenium ni kilomita 4,835; umbali wa kaskazini-kusini ni km. 1,973.

Eneo hili liko katikati ya Hawaii na Australia.

Karibu visiwa vyote havipiti kimo cha mita 2 juu ya UB. Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani na kupanda kwa uwiano wa bahari wataalamu wamekadiria ya kwamba nchi itazama kabisa katika hii karne ya 21.

Lugha na dini hariri

Kuna lugha mbili tu nchini Kiribati, zote mbili zikiwa lugha rasmi, yaani Kiingereza na hasa Kikiribati.

Upande wa dini, linaongoza Kanisa Katoliki (56%), likifuatwa na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti.

Tazama pia hariri


  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.