Nauru ni nchi ya kisiwani ya Mikronesia katika Pasifiki ya kusini.

Nauru


Ni nchi ndogo sana (ya tatu baada ya Vatikani na Monaco), yenye km² 21 pekee na wakazi wasiofikia 10,000.

Kisiwa jirani zaidi ni Banaba katika Kiribati chenye umbali wa km 300.

Nauru haina mji mkuu rasmi.

Historia hariri

Nauru imekaliwa na mchanganyiko wa watu kutoka Polynesia na Mikronesia tangu karne nyingi (miaka 3,000 hivi).

Katika karne ya 19 kisiwa kilitwaliwa na Ujerumani kama sehemu ya makoloni yake ya Pasifiki.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kilikuwa eneo lindwa chini ya Umoja wa Mataifa (UM) na utawala ulikuwa mikononi mwa nchi tatu: Australia, New Zealand na Uingereza.

Uhuru ulipatikana tangu 1968.

Watu hariri

Wakazi wengi (58%) ni wenyeji, wakifuatwa na watu kutoka visiwa vingine vya Pasifiki (26%), Wazungu (8%) na Wachina (8%).

Karibu wote (95%) ni wanene mno, hivyo hali ya afya si nzuri, hasa upande wa kisukari (40%).

Lugha hariri

Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Nauru: Kiingereza (lugha rasmi), Kinauru (lugha ya mawasiliano), na pijini inayounganisha Kiingereza, Kichina na Kiaustronesia.

Dini hariri

Wakazi wengi ni Wakristo (Waprotestanti na Wakatoliki kwa uwiano wa 2:1), wakifuatwa na wafuasi wa Bahai (10%) na Wabuddha (9%).

Uchumi hariri

Uchumi wa Nauru ulitegemea fosfeti iliyopatikana kisiwani kwa wingi. Kwa miaka kadhaa kisiwa kilikuwa nchi tajiri kabisa. Hadi mwaka 2001 huduma za hospitali zilikuwa bure, hapakuwa na kodi, na watu wengi walikuwa na magari mawili au matatu.

Tangu kumalizika kwa fosfeti hali ya kiuchumi imekuwa ngumu sana. 90% za wananchi wanakosa kazi. Serikali haina pesa za kutosha tena, huduma nyingi zimekwama, hata imeanza kupokea misaada kutoka Australia.

Angalia pia hariri


  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.