Belarus

(Elekezwa kutoka Belarusi)

Belarus (kwa Kibelarus: Беларусь (Kikyrili) au Biełaruś (Kilatini); kwa Kirusi:Белоруссия ) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki inayopakana na Urusi, Ukraine, Poland, Lithuania na Latvia.

Рэспубліка Беларусь
Республика Беларусь
Jamhuri ya Belarus
Bendera ya Belarus Nembo ya Belarus
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Belarusian: Мы, беларусы
(Mi Belarusi)
("Sisi Wabelarus")
Lokeshen ya Belarus
Mji mkuu Minsk
53°55′ N 27°33′ E
Mji mkubwa nchini Minsk
Lugha rasmi Kibelarus, Kirusi
Serikali Jamhuri
Alexander Lukashenko
Roman Golovchenko
Uhuru
Ilitangazwa
ilianzishwa
ilikamilishwa

27 Julai 1990
25 Agosti 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
207,600 km² (ya 84)
kidogo sana (183 km²)[1]
Idadi ya watu
 - 2016 kadirio
 - 2009 sensa
 - Msongamano wa watu
 
9,498,700 (ya 93)
9,503,807
45.8/km² (ya 142)
Fedha Rubel ya Belarus (BYN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
FET (UTC+3)
FET (UTC+3)
Intaneti TLD .by
Kodi ya simu +375

-


Ramani ya Belarus

Mji mkuu ni Minsk na miji mingine ni pamoja na Brest, Grodno, Gomel, Mogilev na Vitebsk.

Idadi ya wakazi inapungua: ni watu 9,498,700 (2016).

Historia

hariri

Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.

Wakazi na utamaduni

hariri

Wakazi walio wengi ni Wabelarus (83.7%) ambao wanaongea ama Kibelarus au Kirusi ambavyo vyote viwili ni lugha rasmi. Lugha hizi mbili zina asili moja. Takriban 11% za wakazi ni Warusi.

Kuna pia vikundi vidogo vinavyotumia lugha za pekee kama vile Kipoland, Kiukraine, Kilatvia, Kilituanya na nyingine.

Walio wengi ni wafuasi wa Ukristo katika Makanisa ya Kiorthodoksi (48.3%) na katika Kanisa Katoliki (7.1%).

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Tourism". Belarusian Chamber of Commerce and Industry. Information Site. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-13. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2006.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Belarus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.