Benvenuto Scotivoli

Benvenuto Scotivoli (Ancona, Marche, Italia, 1188 hivi - Osimo, Marche, 22 Machi 1282) alikuwa askofu wa Osimo katika karne ya 13.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Martin IV.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha

hariri

Benvenuto alizaliwa Ancona, Dola la Papa, leo Italia ya Kati, akasomea sheria kwenye chuo kikuu huko Bologna, akiwa na Silvesta Guzzolini, ambaye pia ni mtakatifu.

Alipata kuwa shemasi mkuu wa Ancona kabla hajachaguliwa kuwa askofu.[2]

Alijitahidi kupatanisha wananchi waishi kwa amani.

Haieleweki kama alijiunga na shirika la Ndugu Wadogo, lakini aliamua kufa akiwa amelala ardhini akaomba kuzikwa amevikwa kanzu ya Wafransisko.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.