Charles de Foucauld
Charles Eugène de Foucauld (Strasbourg, 15 Septemba 1858 – Tamanrasset, 1 Desemba 1916) alikuwa mmonaki na padri Mkatoliki kutoka Ufaransa aliyekwenda kuishi peke yake kati ya Watuareg wa Sahara katika nchi ya Algeria ya leo hadi alipouawa[1].
Papa Benedikto XVI alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Novemba 2005, Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 15 Mei 2022.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Desemba.
Maisha
haririKabla ya uongofu wake mwishoni mwa Oktoba 1886, Charles alikuwa ofisa wa Jeshi la Ufaransa huko Moroko, alipoanza kuguswa na mambo ya dini.[2]
Mwaka 1890 alijiunga na Watrapisti lakini aliwaacha mwaka 1897 ili kufuata wito mwingine wa pekee zaidi.
Baada ya kuishi peke yake karibu na Waklara wa Nazareti, mwaka 1901 alipata upadirisho akaenda kuishi jangwani.
Aliuawa mwaka 1916 nje ya ngome aliyojenga ili kulinda Watuareg na anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mfiadini.
Ingawa akiwa hai hakupata wafuasi, mfano na maandishi yake vilichangia uanzishaji wa mashirika na vyama kadhaa duniani kote, kama vile Ndugu Wadogo wa Yesu, Dada Wadogo wa Yesu na Ndugu Wadogo wa Injili.
Maandishi
hariri- Reconnaissance au Maroc, 1883-1884. 4 vols. Paris: Challamel, 1888.
- Dictionnaire Touareg–Français, Dialecte de l'Ahaggar. 4 vols. Paris: Imprimerie nationale de France, 1951-1952.
- Poésies Touarègues. Dialecte de l'Ahaggar. 2 vols. Paris: Leroux, 1925-1930.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90041
- ↑ Vicar. "Visitor information". Retrieved on 22 May 2013.
Viungo vya nje
hariri- Lay Fraternity Ilihifadhiwa 8 Novemba 2016 kwenye Wayback Machine., Lay Fraternity Page
- Facebook Group, Brother Charles' Facebook page
- Lay Fraternity in Canada, Canadian Lay Fraternity Page
- Association Famille Spirituelle Charles de Foucauld (Spiritual Family of Charles de Foucauld)
- Názáret, a Hungarian website about Charles de Foucauld and his spirituality
- "Charles de Foucauld" Ilihifadhiwa 28 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine. at Jesus Caritas
- "Books by or about Charles de Foucauld" Ilihifadhiwa 22 Mei 2016 kwenye Wayback Machine. at Jesus Caritas
- Charles de Foucauld katika Find A Grave
Marejeo mengine
hariri- Casajus, Dominique (1997). "Charles de Foucauld et les Touaregs, Rencontre et Malentendu". Terrain 28: 29-42.
- Casajus, Dominique (2009). Charles de Foucauld: Moine et Savant. CNRS Éditions. ISBN 9782271066312.
- Chatelard, Antoine (2000). La Mort de Charles de Foucauld. Karthala Editions. ISBN 9782845861206.
- Fournier, Josette (2007). Charles de Foucauld: Amitiés Croisées. Éditions Cheminements. ISBN 9782844785695.
- Galand, Lionel (1999). Lettres au Marabout. Messages Touaregs au Père de Foucauld. Paris, Belin, 1999.
- Wright, Cathy (2005). Charles de Foucauld - Journey of the Spirit. Pauline Books and Media. ISBN 9780819815767.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |