Muhimbili
Muhimbili ni mahali maarufu jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa jumla, hasa kutokana na hospitali na chuo kikuu vinavyopatikana huko. Ipo barabara ya Umoja wa Mataifa mtaa wa Upanga Magharibi.[1]
Historia
haririChanzo cha Muhimbili ni Hospitali ya Sewa Haji iliyoanzishwa mwaka 1897 na mfanyabiashara Sewa Haji Paroo kutoka Bagamoyo aliyegharimia ujenzi na kuiachia mali ya kutosha kuiendesha katika wosia wake. Iliendeshwa na serikali ya kikoloni ya Kijerumani kutokana na mali hiyo[2].
Mwaka 1919 ilikabidhiwa mikononi mwa serikali ya kikoloni ya Waingereza walioendelea kuiendesha kama hospitali kwa Waafrika. Mwaka 1956 majengo yaliongezeka yaliyofunguliwa rasmi kama "Dar Es Salaam General Hospital" na Margaret binti wa mfalme wa Uingereza[3] na muda mfupi baadaye ilipokea jina la "Princess Margaret Hospital".
Baada ya uhuru ilipata jina la "Muhimbili", ambalo limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.
Chuo kikuu cha Muhimbili kilianzishwa mwaka 1963: kilifunguliwa kama "Chuo cha Afya Dar es Salaam" ndani ya hospitali iliyoitwa awali Princess Margaret Hospital na wanafunzi 10 waliofuata kozi za uganga au upasuaji.
Mwaka 1968 kikafanywa ni kitengo cha tiba katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Tangu 2007 imeandikishwa kama Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (kwa Kiingereza: Muhimbili University of Health and Allied Sciences; kifupi: MUHAS[4]).
Leo hii Muhimbili ina shule ya madaktari, wauguzi, mafamasia, waganga wa meno, maafisa afya mazingira, maafisa mazingira na elimu ya juu ya afya.
Marejeo
hariri- ↑ Chuo Kikuu cha Muhimbili (2017). "Historia ya chuo kikuu cha Muhimbili". Dar es Salaam. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-11. Iliwekwa mnamo 1 Juni 2018.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); Unknown parameter|=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ <nowiki> Kutoka maktaba: Sewa Haji Paroo, muasisi wa hospitali ya Muhimbili, blogu ya Issa Michuzi, 01.07.2012, iliangaliwa Februari 2021
- ↑ Picha ya Margaret kwenye uzinduzi ya majengo, matini: Princess Margaret 1956 Tour Of Africa Tanganyika (now Tanzania) 11 October 1956 Princess Margaret Opens The Dar Es Salaam General Hospital ; iliangaliwa Februari 2021
- ↑ "Chuo Kikuu cha Muhimbili | Chuo Kikuu cha Muhimbili". www.muhas.ac.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-06. Iliwekwa mnamo 2019-11-06.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help)
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Muhimbili kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |