Mgongo wa bahari ya Pasifiki Mashariki

(Elekezwa kutoka East Pacific Rise)

Mgongo wa bahari ya Pasifiki Mashariki ni mgongo bahari kwenye mashariki ya Bahari Pasifiki takriban kilomita 3000 kutoka pwani ya Amerika Kusini. Ni kama safu ya milima ya volkeno kwenye sakafu ya bahari. Urefu wake ni mnamo km 10,000 ikielekea kutoka kaskazini kwenda kusini.

Mgongo wa bahari ya Pasifiki Mashariki unaonekana kama mkia mwenye mwelekeo wa kaskazini-kusini.

Mgongo huu unafuata mpaka kati ya Bamba la Pasifiki na mabamba gandunia jirani ya Amerika Kaskazini, Cocos, Nazca na Antaktiki.

Kwenye mipaka ya bamba hilo kuna nyufa ambako magma moto kutoka koti la Dunia inapanda juu na kufanya mgongo kama safu ya milima ikiganda katika maji ya bahari. Kwenye mstari huu pande za ganda la Dunia zinaachana. Kasi ya mwendo wa kuachana ni kubwa karibu na kisiwa cha Pasaka (zaidi ya milimita 150 kwa mwaka)[1] , lakini kwenye sehemu za kusini za ufa ni mm 60 pekee[2][3].

Upande wa mashariki wa ufa mabamba ya Cocos na Nazca yanasukumwa na mwendo huu kugonga bara la Amerika ya Kusini na ya Kaskazini ilhali yanazama chini ya mabamba ya bara na hivyo kusababisha kutokea kwa milima ya Andes na volkeno nyingi kwenye pwani ya magharibi ya Amerika.

Kasi kubwa ya kuachana kwa mabamba kwenye mstari wa ufa inazuia kukua kwa milima mirefu chini ya bahari, pia hakuna bonde la ufa la kati kwenye mgongo huo.[4]

Vyanzo hariri

  1. DeMets, Charles; Gordon, Richard G.; Argus, Donald F. (2010). "Geologically current plate motions". Geophysical Journal International (in English) 181 (1): 52. doi:10.1111/j.1365-246X.2009.04491.x. 
  2. "Understanding plate motions", USGS. Retrieved 26 June 2013.
  3. Britannica
  4. Ken MacDonald: What Is The Mid-Ocean Ridge? Ocean Explorer. National Oceanic and Atmospheric Administration, United States Department of Commerce

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: