Eneo bunge la Msambweni


Eneo bunge la Msambweni ni moja kati ya Majimbo 290 ya Uchaguzi nchini Kenya. Jimbo hili linapatikana katika Kaunti ya Kwale, pwani mwa Kenya, miongoni mwa majimbo manne katika kaunti hiyo. Jimbo la Msambweni lina wodi kumi, zote zikichagua madiwani kwa baraza la Kwale County.

Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi

Historia hariri

Jimbo hili lilianzishwa wakati wa uchaguzi mkuu wa 1988, huku mbunge wake wa kwanza akiwa Kassim Bakari Mwamzandi.

Wabunge hariri

Uchaguzi Mbunge [1] Chama Vidokezo
1988 Kassim Bakari Mwamzandi KANU Mfumo wa Chama Kimoja
1992 Kassim Bakari Mwamzandi KANU
1997 Mwarere Wa Mwachai KANU
2002 Abdalla Jumaa Ngozi NARC
2007 Omar Mbwana Zonga ODM

Kata na Wodi hariri

Kata
Kata Idadi ya Watu*
Diani 60,565
Dzombo 36,118
Kikoneni 17,571
Kingwende/Shira 10,656
Kinondo 20,798
Lunga Lunga 20,101
Mivumoni 10,300
Msambweni 17,104
Mwereni 32,034
Pongwe/Kidimu 15,104
Vanga 13,744
Jumla x
*Sensa ya 1999.
Wards
Wodi Wapiga Kura
Waliojisajili
Diani 15,751
Dzombo 7,571
Kasemeni / Sega 5,665
Kikoneni 4,444
Kingwende/Shirazi 3,836
Kinondo 6,107
Mivumoni / Msambweni 9,136
Mwereni 4,930
Pongwe/Kidimu 5,573
Vanga 4,216
Jumla 67,229
*Septemba 2005 [2].

Tazama Pia hariri

Marejeo hariri