Eneo la ng'ambo la Uingereza

Eneo la ng'ambo la Uingereza ni lolote kati ya maeneo 14 ambayo ni chini ya serikali ya Uingereza lakini si sehemu za nchi.

Ramani ya maeneo ya ng'ambo ya Uingereza
(Eneo la Kiingereza kwenye Antaktika na Akrotiri na Dhekelia (Kupro) havionyeshwi)

Kwa Kiingereza yameitwa "British Overseas Territory" tangu ilipotungwa sheria ya mwaka 2002 badala ya jina la awali "British dependent territory" yalivyoitwa tangu mwaka 1981. Kabla ya 1981 yaliitwa "makoloni"

Hali ya maeneo hayo ni tofauti na ile ya Jumuiya ya Madola ambayo ni jumuiya ya hiari ya baadhi ya makoloni ya zamani ya Uingereza na nchi nyingine zilizopenda kujiunga.

Mambo ya kisheria

hariri

Kwa jumla wakazi wa maeneo ya ng'ambo ya Uingereza ni raia wa Uingereza na wana haki kuhamia Uingereza yenyewe. Kila eneo lina bunge lake na uhuru fulani wa kutunga sheria zake.

Visiwa vya mfereji wa Kiingereza (Jersey, Guernsey) na Isle of Man si maeneo ya ng'ambo ya Uingereza bali "maeneo chini ya taji la Uingereza".

Maeneo ya ng'ambo ya Uingereza

hariri
Bendera Eneo Mahali Wito Eneo Wakazi Mji Mkuu
  Anguilla Karibi Strength and Endurance 91 km²
(35.1 mi²)
14,869 The Valley
  Bermuda Atlantiki Quo fata ferunt (Kilatini: "Kote heri inakotupeleka") 54 km²
(20.8 mi²)
62,506 Hamilton
  Eneo la Uingereza katika Antaktika Antarctica Research and discovery 1,709,400 km²
(666,000 mi²)
50/400 staff Rothera (kituo kikuu)
  Eneo la Uingereza katika Bahari Hindi Bahari Hindi In tutela nostra Limuria (Kilatini: "Tumekabidhiwa Limuria") 60 km²
(23 mi²)
3,000 military and staff Diego Garcia (kituo cha kijeshi)
  Visiwa vya Virgin vya Uingereza Karibi Vigilate (Kilatini: "Mwe macho!") 153 km²
(59 mi²)
31,758 Road Town
  Visiwa vya Cayman Karibi He hath founded it upon the seas 264 km²
(101.9 mi²)
68,076 George Town
  Visiwa vya Falkland Atlantiki Desire the right 12,173 km²
(4,702 mi²)
3,377 Stanley
Gibraltar Ulaya ya Kusini Nulli expugnabilis hosti (Kilatini: "Haishindwi na adui yeyote") 6.5 km²
(2.5 mi²)
33,701 Gibraltar
  Montserrat Karibi 101 km²
(39 mi²)
5,215 Plymouth
  Visiwa vya Pitcairn Pasifiki 47 km²
(18 mi²)
50 Adamstown
  Saint Helena, Ascension na Tristan da Cunha Atlantiki Loyal and unshakeable 420 km²
(162 mi²)
5,633 Jamestown
  Visiwa vya South Georgia na South Sandwich Atlantiki Leo terram propriam protegat (Kilatini: "Simba alinda kwake") 3,903 km²
(1,507 mi²)
99 staff King Edward Point/Grytviken
  Akrotiri and Dhekelia (Kupro) Mediteraneo (Kupro) Dieu et mon droit (Kifaransa: "Mungu na haki yangu") 255 km²
(98 mi²)
7,700 + wanajeshi 8,000 Episkopi Cantonment
  Visiwa vya Turks na Caicos Karibi One people, one nation, one destiny 430 km²
(166 mi²)
38,191 Cockburn Town

Viungo vya Nje

hariri