Revocatus (kutoka Kilatini "revocare" - kuita tena) ni mmoja wa mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa tarehe 7 Machi 203 mjini Karthago wakati wa dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Kifodini cha Mt. Perpetua na wenzake katika vioo vya kanisa la Bikira Maria huko Vierzon (karne ya XIX).

Anaheshimiwa tangu kale kati ya watakatifu wafiadini pamoja na watakatifu Perpetua na Felista wanaojulikana zaidi kama mashahidi Wakristo wa Afrika ya Kaskazini.

Revocatus alikuwa kati ya watumwa wa familia ya Perpetua sawa na mwenzake Felista. Pamoja na wasichana hao na Saturninus alikuwa mmoja wa wanafunzi wa imani ya kikristo mjini Karthago waliojiandaa kubatizwa. Kundi lote likakamatwa pamoja na kutupwa jela. Jinsi ilivyokuwa kawaida walipewa nafasi ya kuachana na Ukristo lakini wote walisimama imara wakabatiwza gerezani.

Pamoja na akina mama hao vijana na wanaume wengine 3 walikamatwa pamoja na kutupwa jela. Jinsi ilivyokuwa kawaida walipewa nafasi ya kuachana na Ukristo lakini wote walisimama imara wakabatiwza gerezani.

Walihukumiwa adhabu ya kifo katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori. Waliraruliwa na wanyama mbalimbali, wakamalizwa kwa upanga, isipokuwa Sekondinus aliyefariki gerezani.

Revocatus anakumbukwa kwamba alisimama mbele ya umati wa watu waliokuja kuona damu ya wafiadini hao akawakumbusha ya kuwa kila mmoja atawajibika mbele ya Mungu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifodini chao[1].

Jina la Revocatus limekuwa linatumiwa na Wakatoliki wa Afrika ya Mashariki.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.