Fidelis wa Sigmaringen

Fidelis wa Sigmaringen (157824 Aprili 1622) alikuwa padri mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo, katika tawi la Wakapuchini.

Fidelis wa Sigmaringen.

Ametambuliwa na Papa Benedikto XIII kuwa mwenye heri tarehe 24 Machi 1729, halafu Papa Benedikto XIV alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 29 Juni 1746.

Sikukuu yake ni 24 Aprili[1].

Maisha

hariri

Fidelis alizaliwa katika mji wa Sigmaringen upande wa Kusini-Magharibi wa Ujerumani, mwaka 1578. Jina lake lilikuwa Mark Roy.

Alisomea Freiburg falsafa na sheria akawa wakili maarufu hasa kwa kuwatetea watu fukara.

Baadaye akajiunga na Wakapuchini, akaishi maisha magumu ya toba, makesha na sala.

Alijulikana kuwa mhubiri asiyechoka, hivyo akatumwa Uswisi hasa kwa lengo la kurudisha Waprotestanti katika Kanisa Katoliki, akawa na mafanikio makubwa hadi alipouawa na wapinzani wake mwaka 1622 mjini Seewis, akiwa anatoka katika adhimisho la Misa.

Ni mfiadini wa kwanza wa Idara ya Uenezaji wa Injili ya Kanisa Katoliki.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Alban Butler, Vol. IV of "The Lives or the Fathers, Martyrs and Other Principal Saints". 1864 edition published by D. & J. Sadlier, & Company
  • Acts of the canonization of SS. Fidelis of Sigmarengen, Camillus de Lellis, Peter Regalati, Joseph of Leonissa and Catherine Ricci, by Pope Benedict XIV., printed in 1749, folio. On St. Fidelis, pp. 101, 179, and the bull for his canonization, p 516.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.