Galileo (kipimaanga)

Galileo ilikuwa kipimaanga kilichorushwa na NASA mwaka 1989 kwa shabaha ya kufanyia utafiti sayari ya Mshtarii (Jupiter) na miezi yake. Iligundua sayari ya Jupita na mwezi wake. Ilifika Mshtarii mnamo 1995.

Galileo mbele ya Mshtarii na Io kwa macho ya msanii.
Njia ya Galileo kwenda Mshtarii na kuizunguka
      Galileo ·      Mshtarii ·      Dunia ·      Zuhura ·      951 Gaspra.

Sehemu ya kwanza ya kipimaanga ilitengwa kwenye Julai 1995 na kuelekea Mshtarii.[1] Ikafika kwenye Desemba 1995 ikaingia katika angahewa ambako iliweza kukusanya data kwa dakika 57 hadi kuharibika.

Sehemu kuu ikaingia katika obiti ya Mshtarii ikazunguka muda wa miezi 9 ikashuka kwenye angahewa ya sayari ambako iliangamizwa mnamo 21 Septemba 2003. [2]

Jina lilichaguliwa kwa kuheshimu Galileo Galilei, mmoja kati ya wanaastronomia bora wa nyakati zote.

MarejeoEdit

  1. NASA: Solar System Exploration: Missions: By Target: Jupiter: Past: Galileo. NASA. Iliwekwa mnamo 2011-03-29.
  2. NASA: Solar System Exploration: Galileo Legacy Site. NASA. Iliwekwa mnamo 2011-03-29.