Martinique

département ya Ufaransa

Martinique (kwa Kifaransa; kwa Krioli: "Matinik" au "Matnik") ni kisiwa cha Antili Ndogo katika Bahari ya Karibi. Ni eneo la ng'ambo la Ufaransa na mkoa (departement) wa Ufaransa. Hivyo ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.

Uwanja wa ndege wa Martinique








Martinique

Bendera
Nchi Bendera ya Ufaransa Ufaransa
Mji mkuu Fort-de-France
Eneo
 - Jumla 1,128 km²
Idadi ya wakazi (2016)
 - Wakazi kwa ujumla 376,480
Tovuti:  http://www.cr-martinique.fr/
Ramani ya Martinique.

Eneo lake ni km² 1,128.

Makao makuu ni Fort-de-France. Miji mingine ni pamoja na Sainte-Anne na St. Pierre (iliyoharibiwa na mlipuko wa volkeno ya Mont Pelee mwaka 1902).

Idadi ya wakazi ni 376,480. Takriban 83% ni wa asili ya Afrika au machotara wa aina mbalimbali. Wazee wao waliletwa huko kama watumwa kwa ajili ya kazi katika mashamba ya miwa. Kikundi kikubwa cha pili ni Wahindi (10%), Wazungu (6%). Waliobaki ni Waarabu, Wachina n.k.

Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wengi wanaongea pia Krioli yenye asili ya Kifaransa ambayo hata hivyo haieleweki tena na Wafaransa wa Ulaya.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo: 86% ni Wakatoliki, 5.6% Waprotestanti.

Utamaduni

hariri

Martinique ni maarufu kwa muziki wake wa zouk. Mwanamuziki mashuhuri wa aina hii ni Kassav.

Tazama pia

hariri
  • Guadeloupe, eneo lingine la Ufaransa katika Bahari ya Karibi

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali
Taarifa za jumla
Safari
  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Martinique kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.