Hifadhi ya Katavi

(Elekezwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Katavi)

Hifadhi ya Katavi ni moja ya hifadhi za taifa iliyoundwa mwaka 1974.

Hifadhi ya Taifa ya Katavi, nyakati za jioni
Viboko: mama na mtoto.
Picha ya mamba

Iko juu ya uwanda mpana wa mafuriko magharibi mwa Tanzania katika mkoa wa Katavi na mkoa wa Rukwa. Hifadhi hiyo inazo takribani kilomita za mraba 4,471 (maili za mraba 1,726) katika eneo hilo, ambayo inakuwa ni hifadhi ya tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.

Ni hifadhi ya mbali sana ambayo hutembelewa mara kwa mara kuliko viwanja vingine vya Tanzania. Hifadhi hiyo inahusisha mto Katuma na msimu wa Ziwa Katavi na Ziwa Chada.

Mandhari kuu katika hifadhi

hariri
  • Maeneo ya majimaji yenye majani
  • Mimea jamii ya mitende na
  • Mto Katuma

Hifadhi hii inasifika kwa:

Pia wanyama kama simba na chui hawana shida ya mawindo kwani katika himaya yao kuna makundi ya swala, nyamela topi wa miguu mieupe, pundamilia na nyati.

Kuna aina zipatazo 400 za ndege waliozagaa katika miti ya acacia, kingo za mto, mabwawa na makundi kadhaa ya mwari (pelicans) yanayoambaa ziwani. Ni kawaida kuyaona makundi makubwa ya tembo yakila majani katika mabwawa, huku miili yao ikiwa imefunikwa na maji na magugu.

Namna ya kufika katika hifadhi

hariri

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.