Hoteli za Serena (kwa Kiingereza: Serena Hotels) ni mnyororo wa hoteli unaofanya kazi nchini Afghanistan, Kenya, Msumbiji, Pakistan, Rwanda, Tanzania na Uganda. Ni moja ya makampuni 96 yaliyo chini ya Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED), ambayo ni shirika la kutoa faida kwenye Aga Khan Development Network (AKDN). Kibiashara, wao hutumia jina la Tourism Promotion Services (TPS Serena). Kampuni hii imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi na ina majumba 19 katika bara la Afrika.

Hoteli za Serena
Ilipoanzishwa1970s in Kenya
Makao MakuuNairobi, Bendera ya Kenya Kenya
Owner(s)Tourism Promotion Services
Tovutihttp://www.serenahotels.com/index.asp

Historia hariri

Hoteli ya Serena mjini Nairobi ni yenye nyota tano na ndio hoteli kuu katika kundi la Hoteli za Serena. Ina vyumba 183 na vyumba 7 vya waheshimiwa, pamoja na chumba kimoja cha rais au mkuu wa nchi. Kituo chake cha Maisha Health Club ni bora zaidi nchini Afghanistan. Serena ni mwanachama wa Leading Hotels of the World (Hoteli zinazoongoza kote duniani).

Serena Hotel iliyomo mjini Islamabad, Pakistan ilibuniwa na mbunifu maarufu Nayyar Ali Dada na kufunguliwa mwaka 2002. Ina vyumba 220, pamoja na chumba cha densi ya watu 200, mikahawa mitatu, maduka ya kununua vitu, na klabu ya afya na bwawa la kuogelea. Dari la juu la hoteli pamoja na uwanja wake unaweza kuchukua wageni 1,000 kwenye karamu. Hii pia ni mwanachama wa Leading Hotels of the World.

Hoteli ya Kampala Serena ni ya nyota 5 iliyozungukwa na bustani la kuvutia. Hoteli hii ina kituo cha kushukia helikopta. Ina makao 152 ya kibinafsi, pamoja na vyumba vya kisasa 32 na vyumba vya waheshimiwa 12,ikiwemo moja ya rais. Hoteli hii ilimkaribisha Malkia Elizabeth II wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Madola ya Wakuu wa Serikali mnamo 2007 (CHOGM 2007). [1] Karibu na hoteli hii kuna Kampala Serena International Conference Center iliyo na viti 1500 wajumbe na yenye uwezo wa kutafsiri lugha tisa.[2]

Mapema mwaka 2007, Serena ilichukua usimamizi wa majumba mawili nchini Rwanda kutoka Southern Sun. Hoteli hizi zimebadilishwa majina na kuwa Kigali Serena Hotel na Ziwa Kivu Serena Hotel.

Serena Hotel Kabul mjini Kabul, Afghanistan ilifunguliwa mwaka 2005. Tarehe 14 Januari 2008, The Serena hoteli iliyopo mjini Kabul, Afghanistan ilikuwa shabaha la mashambulizi ya wapiganaji, pamoja na mabomu. Watu saba waliuawa katika shambulio hilo, ikiwa ni pamoja na mwandishi wa habari Kinorwe na wa Marekani.[3] Taliban walidai wajibu wao wa vita hivi.


Mali ya Serena barani Afrika hariri

Mali ya Serena barani Asia hariri

 
Mlango wa Hoteli ya Serena Kabul, Afghanistan.

Angalia pia hariri

Marejeo hariri

  1. Kuhusu Kampala Serena Hotel. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-01-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-05.
  2. Kuhusu Kampala Serena International Conference Center. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-01-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-05.
  3. Serena Hotel Kabul Attacked mwaka 2008

Viungo vya nje hariri