Medici
(Elekezwa kutoka House of Medici)
Medici ni jina la familia ya Firenze katika Italia ya Kati iliyokuwa muhimu upande wa siasa, uchumi na utamaduni, hasa wakati wa karne ya 15 na 16 BK.
Mapapa watatu wa Kanisa Katoliki walikuwa wa ukoo huo, pamoja na watawala mbalimbali za mji wa Firenze; watoto wao walioa au kuolewa katika familia za wafalme wa Ulaya.
Walijenga utajiri katika biashara ya kitambaa wakaendelea kuunda benki kadhaa zilizokuwa aina mpoya ya biashara wakati ule. Uwezo wao wa kiuchumi waliutumia baadaye kisiasa.
Watawala na Mapapa wa ukoo wa Medici waliajiri wasanii wengi na kugharimia pia wataalamu, hivyo wakajenga kipindi cha utamaduni wa juu cha Italia kilichong'aa kote Ulaya.
Akina Medici mashuhuri
hariri- Salvestro de' Medici (1331 – 1388) alikuwa wa kwanza wa familia aliyetawala Firenze hadi 1382
- Giovanni di Bicci de' Medici (1360 – 1429) aliongeza utajiri wa nyumba hadi kuwa familia tajiri ya Ulaya
- Cosimo Mzee (1389 – 1464) alianzisha mfululizo wa watawala wa Medici wa Firenze
- Lorenzo de' Medici (1449 – 1492) mtawala wa Firenze aliyetumia pesa nyingi kwa sanaa
- Giovanni de' Medici (1475 – 1523) alipata kuwa Papa Leo X
- Giulio de' Medici (1478 – 1534) alipata kuwa Papa Klementi VII
- Cosimo I de' Medici (1519 – 1574) aliendelea kuwa mtemi wa Toscana
- Catherine de' Medici (1519 – 1589), malkia wa Ufaransa
- Alessandro Ottaviano de' Medici (1535 – 1605) alijulikana kama Papa Leo XI
- Marie de' Medici (1575 – 1642) alikuwa malkia wa Ufaransa
- Anna Maria Luisa de' Medici (1667 – 1743) alikuwa mtemi wa Toscana na mwisho wa familia ya Medici aliyeaga dunia bila watoto.
Viungo vya Nje
hariri- Outline of the history of the Medici family
- Genealogical manuscript on the house of the Medici
- (Kijerumani) Genealogical tree of the house of the Medici
- Galileo and the Medici Family at PBS
- Adrian Fletcher’s Paradoxplace – 3 pages of Medici portraits and history Ilihifadhiwa 16 Juni 2012 kwenye Wayback Machine.
- Medici Archive Project
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Medici kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |