Immanuel Kant
Immanuel Kant alikuwa mwanafalsafa Mjerumani kutoka milki ya Prussia. Anahesabiwa kati ya wanafalsafa muhimu zaidi wa zama za mwangaza.
Immanuel Kant | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 22 Aprili 1704 |
Alikufa | 12 Februari 1804 |
Nchi | Prussia (Ujerumani) |
Kazi yake | profesa wa chuo kikuu mwanafalsafa |
Maisha Edit
Kant alizaliwa mjini Königsberg (sasa: Kaliningrad) kama mtoto wa fundi. Mamake alimsomesha kweye shule ya sekondari akaendelea kusoma tholojia, falsafa, sayansi, fizikia na hisabati. Tasnifu (thesis) yake ya kwanza haikupokelewa na profesa wake mwaka 1746 hivyo alifanya kazi ya mwalimu kwenye nyumba ya matajiri na makabaila mbalimbali kwenye mazingira ya Königsberg.
1754 alirudi kwenye chuo kikuu akamaliza masomo yake. Tangu 1755 alikuwa mwalimu na tangu 1870 profesa kamili kwenye chuo kikuu cha Königsberg.
Hakuoa aliishi na mtumishi wa nyumbani tu hadi kifo chake mwaka 1804 kwa umri wa miaka 80. Kaburi lake ni kando la kanisa kuu la Königsberg limetunza hata siki hizi baada ya kufukuzwa kwa Wajerumani na kuwa sehemu ya Urusi.
Falsafa Edit
Mwanafalsafa wa mwangaza Edit
Kwa Kant kazi ya akili inaanza kwa kufikiri mwenyewe. Alisema "Sapere aude!" na hii inamaanisha : "Usiogope kutafakari mwenyewe". Aliona ni muhimu ya kwamba kila mtu anatumia akili yake mwenyewe badala ya kutegemea mawazo ya watu wengine. Mawazo na mafundisho yote yanapaswa kupitia kwenye uhakiki wa akili.
Kwa njia hii alitafsiri mwelekeo wa zama za mwangaza na wengi wanamwona kuwa alikamilisha jitihada za mwangaza. Kant aliandika: "Mwangaza inamaanisha kuondoka kwa binadamu kutoka uchanga wake uliosababisha mwenyewe. Uchanga unamaanisha kutotumia akili bila mwongozo wa mwingine. Uchanga huu husababishwa na mtu mwenyewe si kwa sababu ya uhaba wa akili lakini kwa sababu ya uhaba wa nia na hofu ya kutumia akili bila mwongozo wa mwingine."
Ngazi ya urazini Edit
Katika kutafakari kwake Kant alipita njia. Mara nyingi hii inagawiwa katika vipindi viwili: labla ya "uhakiki" na baada ya "uhakiki"". Tangu kutunga kitabu chake cha "Uhakiki wa akili tupu" alifundisha tofauti kuliko awali. Katika kipindi cha kwanza hadi 1860 alifuata mtindo wa walimu wake uliotiwa urazini (rationalism). Alirudia jinsi alivyofundishwa na wanafalsafa kama Leibnitz ya kwamba akili inaweza kutambua kila kitu.
Ngazi ya Uhakiki Edit
Katika tasnifu yake alianza kusogea mbali na urazini unaofundisha ya kwamba akili inaweza kutambua ulimwengu na hali halisi ya vitu vyote. Kant alisisitiza ya kwamba si akili peke yake lakini pia maarifa na ufahamu. Kuona ni muhimu kama kutafakari.
Kazi ya falsafa aliona katika kufikiria uhusiano wa yale yanayopatikana akilini kama dhana na yale yanayonekana hali halisi katika mazingira ya mtu. Msingi huu ulikuwa mpya ukalazimisha kutafakari upya maswali mengi katika falsafa hasa metafizikia.
Baada ya kupokea wito la kuwa profesa Kant alikuwa na kipindi nyamavu cha miaka 10 maana yake alifundisha wanafunzi wake lakini hakutoa kitabu kipya akitafakari yale yanayofuata kutokana na msingi wake mpya.
Alihitaji kulijibu swali jinsi gani binadamu anapata ujuzi wake na jinsi gani akili inaweza kuushughulikia.
Maswali 4 ya Kant Edit
Kant alijiuliza maswali manne:
1. Ninaweza kujua nini? 2. Ninatakiwa kufanya nini? 3. Ninweza kutumaini nini? 4. Binadamu ni nini ?
Uhakiki wa akili tupu Edit
Mwaka 1871 alitoa kitabu cha "uhakiki wa akili tupu". Humo aliuliza swali je akili inaweza kujua nini bila maarifa.
Anaangalia ujuzi wa "a priori" (Kilatini: kutoka chanzo). KUna mambo ambayo tunajua bila maarifa na ujuzi huu ni msingi wa kupata maarifa. Tunajua kuwepo kwa wakati na mahali bila kuiona - na kw aujuzi huu ndani yetu hatuwezi kuelewa wakati fulani au mahali fulani. Hapa anaita hisabati aina ya "sayansi a priori" kwa sababu dhana zote za hisabati ziko bila maarifa yoyote.
Halafu antazama mipaka ya akili. Akili inataka kuendelea lakini inagonga mipaka. Maswali kama: Je kuna roho ndani ya mtu isiyokufa? Kuna Mungu? Dunia haina mipaka? yanahusu mambo ambayo akili haiwezi kujibu kwa uhakika. Hakuna uthebitisho kwa namna ya uthebitisho wa kisayansi.
Uhakiki wa akili tendaji Edit
"Uhakiki wa akili tendaji" ni kitabu cha pili kinachoendeleza kile cha kwanza. Akili tendaji ni matumizi ya akili kwa maadili ya kutenda yale ambayo ni mema na sahihi.
Hapa anafundisha "amri halisi": "Katika matendo yako fuata shabaha hizi tu zinazofaa kuwa msingi wa sheria kwa watu wote."
Viungo vya Nje Edit
- Works by Immanuel Kant in audio format from LibriVox
- Immanuel.Kant,Critique of Pure Reason (1787 (english)
- Internet Encyclopaedia of Philosophy The Internet Encyclopaedia of Philosophy has several topics about Kant
- Immanuel Kant in Italia A Website on the presence and diffusion of the philosophy of Immanuel Kant in Italy
- Stephen Palmquist's Glossary of Kantian Terminology Archived 2 Novemba 2009 at the Wayback Machine.
- Kant's Categories as grammatical reifications Archived 21 Septemba 2009 at the Wayback Machine.
- Kant's Ethical Theory Kantian ethics explained, applied and evaluated
- Kant & Ethics Archived 11 Oktoba 2007 at the Wayback Machine. Extensive links and discussions from Lawrence Hinman at University of San Diego
- Notes on Deontology A conveniently brief survey of Kant's deontology
- Kant's Ethics in Italy today Contemporary Italian writings about Kant's Ethics
- North American Kant Society (NAKS) Archived 30 Juni 2007 at the Wayback Machine.
- Kant on the Web Archived 26 Oktoba 2009 at the Wayback Machine. on Stephen Palmquist's website
- Kant Links
- Kant's Epistemology and Metaphysics according to the Friesian school
- Kant and the project of enlightenment Archived 15 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- German Idealist Foundations of Durkheim's Sociology and Teleology of Knowledge
- Several Kant's works in clickable pdf Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Routledge Encyclopedia of Philosophy (14 sections on Kant)
- International Kant Interview - 2004 Archived 5 Aprili 2010 at the Wayback Machine.
- Readable versions of Prolegomena, Groundwork for the Metaphysic of Morals, and Critique of Pure Reason
- All works of Kant (German) Archived 1 Novemba 2014 at the Wayback Machine.
- Kant's moral philosophy and the question of pre-emptive war, Revue Sens Public Archived 2 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
- Kant in the Classroom Archived 3 Septemba 2009 at the Wayback Machine. (background information for Kant's lectures)
- Immanuel Kant's works: text, concordances and frequency list
- Kant On Race and Development Archived 17 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
- Michel Foucault's Dissertation on Kant's Anthropology
- Kant on property
- Part one of 'The Critique of Aesthetic Judgment' Archived 16 Februari 2009 at the Wayback Machine.
- The Stanford Encyclopedia of Philosophy has several entries on Kant:
- Kant's Fourth Critique Italian writings