Eneo bunge la Mbeere Kaskazini
(Elekezwa kutoka Jimbo la Uchaguzi la Siakago)
Eneo bunge la Mbeere Kaskazini (awali: Siakago) ni Jimbo la Uchaguzi nchini Kenya. Ni moja kati ya majimbo mane yaliyo katika Kaunti ya Embu. Jimbo hilo lina wodi tano na zote huwachagua madiwani kwa baraza la Mbeere County.
Jamhuri ya Kenya |
Makala hii imepangwa kwa mfululizo: |
|
Nchi zingine · Atlasi |
Mji wa Siakago ambao ni mji mkuu wa Wilaya ya Mbeere unapatikana katika kata ya Nthawa katika jimbo hili.
Historia
haririJimbo hili lilianzishwa wakati wa uchaguzi mkuu wa 1988 wakati jimbo la Embu Mashariki liligawanywa kutengeneza Jimbo la Runyenjes na Siakago.
Silvester Mate, Mbunge wa kwanza wa Siakago, ndiye alikuwa pia mbunge wa mwisho wa Embu Mashariki baada ya kushinda kiti hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu a 1983[1].
Wabunge
haririUchaguzi | Mbunge [1] | Chama | Vidokezo |
---|---|---|---|
1988 | Silvester Mate | KANU | Mfumo wa Chama Kimoja |
1992 | Gerald Ireri Ndwiga | KNC | Ndwiga alihamuia KANU mnamo 1995 na kushinda uchaguzi mdogo uliofuatia |
1997 | Silas M’Njamiu Ita | DP | Ita aliaga dunia mnamo 1999 [2] |
1999 | Justin Bedan Njoka Muturi | KANU | Uchaguzi Mdogo |
2002 | Justin Bedan Njoka Muturi | NARC | |
2007 | Kivuti Maxwell | Safina |
Kata na Wodi
haririKata | |
Kata | Idadi ya Watu* |
---|---|
Gituburi | 8,005 |
Ishiara | 13,575 |
Kanyuambora | 11,658 |
Kiangombe | 8,294 |
Muminji | 8,390 |
Mutitu | 7,040 |
Ndurumori | 9,750 |
Nthawa | 16,892 |
Jumla | x |
*Hesabu ya 1999. |
Wodi | |
Wodi | Wapiga Kura Waliojisajili |
---|---|
Ishiara | 4,685 |
Kanyuambora | 4,812 |
Kiang'ombe | 6,844 |
Muminji | 5,883 |
Nthawa | 9,808 |
Jumla | 32,032 |
*Septemba 2005 [3].
|
Tazama Pia
haririMarejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 Center for Multiparty Democracy: Politics and Parliamenterians in Kenya 1944-2007 Ilihifadhiwa 28 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Daily Nation, 22 Aprili 1999: Siakago MP dies in hospital
- ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Eneo bunge la Mbeere Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |