Kaunti ya Makueni ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Kaunti ya Makueni
Kaunti
Kaulimbiu: "Haven of Opportunities"

Kaunti ya Makueni katika Kenya
Coordinates: 1°48′S 37°37′E / 1.800°S 37.617°E / -1.800; 37.617
Nchi Kenya
Nambari17
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Mji mkuuWote
Miji mingineEmali, Makindu, Kibwezi, Mtito Andei
Serikali
GavanaProf. Kivutha Kibwana, EGH
Naibu wa GavanaAdelina Mwau Ndeto, OGW
SenetaMutula Kilonzo Junior
Mwakilishi wa wanawakeRose Mumo
BungeBunge la Kaunti ya Makueni
Wawakilishi Wadi30
Maeneo bunge6
Eneo
Jumlakm2 8 169.8 (sq mi 3 154.4)
Idadi ya Watu
Jumla987,653
Msongamano121 /km²
Majira ya SaaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovuti
makueni.go.ke

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 987,653 katika eneo la km2 8,169.8, msongamano ukiwa hivyo wa watu 121 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Wote.

Jiografia

hariri

Kaunti ya Makueni imepakana na Machakos (kaskazini), Kitui (mashariki), Taita Taveta (kusini) na Kajiado (magaribi). Ni kaunti nusu kavu. Tabianchi hii huiwezesha Makueni kuzalisha maembe kwa muda mrefu kwa mwaka.

Mto Athi hupitia katika mpaka wa mashariki. Kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, asilimia 39 ya Makueni ina maji chini ya ardhi[2].

Tambarare ya Yatta huwa katika kaskazini mwa kaunti. Vilima vya Chyulu na Mbuga ya Kitaifa ya Vilima vya Chyulu huwa kusini mwa kaunti.

Utawala

hariri

Kaunti ya Makueni imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[3]:

Eneo bunge Kata
Mbooni Tulimani, Mbooni, Kithungo/Kitundu, Kiteta/Kisau, Waia-Kako, Kalawa
Kilome Kasikeu, Mukaa, Kiima Kiu/Kalanzoni
Kaiti Ukia, Kee, Kilungu, Ilima
Makueni Wote, Muvau/Kikuumini, Mavindini, Kitise/Kithuki, KathonzweniNzau/Kilili/Kalamba, Mbitini
Kibwezi West Makindu, Nguumo, Kikumbulyu North, Kimumbulyu South, Nguu/Masumba, Emali/Mulala
Kibwezi East Masongaleni, Mtito Andei, Thange, Ivingoni/Nzambani

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]

hariri
  • Kathonzweni 79,780
  • Kibwezi 197,000
  • Kilungu 60,952
  • Makindu 84,946
  • Makueni 130,375
  • Mbooni East 97,756
  • Mbooni West 102,594
  • Mukaa 107,549
  • Nzaui 126,701

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. "Hope in Tapping Underground Water in Makueni - Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-02. Iliwekwa mnamo 2018-04-26.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.