Kisii
Kisii ni mji upatikanao Kusini Magharibi mwa Kenya. Huu ndio mji mkubwa wa biashara katika miinuko ya Gusii. Mji huu pia huitwa Bosongo au Getembe
Jiji la Kisii | |
Mahali pa mji wa Kisii katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°41′0″S 34°46′0″E / 0.68333°S 34.76667°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Kisii |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 83,460 |
Tovuti: www.kisii.com |
Kisii ndio makao makuu ya Kaunti ya Kisii. Awali ulikuwa makao makuu ya Wilaya ya Kisii kwa ujumla kabla ya wilaya hiyo kugawanywa na kuzaa Wilaya ya Nyamira na Wilaya ya Gucha. Hata hivyo bado mji huo uliendelea kuzifaidi wilaya hizi na Nyanza kusini kwa ujumla, hasa kibiashara.
Uchumi
haririKuna shughuli za viwanda katika mji huu na vingi vya viwanda hivi vinahusiana na kilimo kwa kuwa Kisii uko katika eneo lililotawaliwa na ukulima.
Pia kuna uchongaji wa madini katika eneo hili, hasa madini ya soapstone katika eneo la Tabaka[1].
Elimu
haririKutokana na idadi kubwa ya watu (83,460 kadiri ya sensa ya mwaka 2009[2]) na ongezeko la mahitaji ya elimu, vyuo vingi vimeanzisha matawi Kisii. Miongoni mwa vyuo vilivyoanzisha matawi mjini ni:
Licha ya hivyo kuna shule nyingi za sekondari humo mjini, kama vile Shule ya Upili ya Kisii.
Wakazi
haririMji huu una wakazi wa matabaka mbalimbali, miongoni mwao wakiwemo Wahindi na Wakikuyu wanaojihusisha na biashara, huku idadi kubwa ikiwa Wakisii.
Hata hivyo, Wahindi wamenunua mali nyingi kutoka kwa Wakisii, ambayo wamekuza kuwa maduka makuu na jambo hili limeukuza mji huu kiajabu hivi karibuni. Leo hii mji huu unajivunia maduka makuu kama Tuskys na Nakumatt, benki kama vile Benki ya Equity, Benki ya Family, K-Rep, Benki ya Cooperative na Benki ya Barclays ambayo yote yameanzisha matawi mjini Kisii.
Hali ya usafi na nyumba
haririMji wa Kisii una kiwango cha chini cha usafirishaji wa takataka na maji machafu. Kituo pekee cha kusafisha maji machafu kilikuwa Daraja Mbili lakini kimehamishwa nje ya mji.
Mji huu pia unakumbwa na uhaba wa ardhi huku mitaa mingi mjini ikianzishwa bila mpango maalumu.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Tabaka la Kisii (Kisii Tribe)-Carvers of Soapstone in Kisii: kenya-information-guide.com Archived 18 Machi 2010 at the Wayback Machine.
- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Viungo vya nje
hariri- Kuhusu Gusii
- Tovuti Rasmi ya Kisii
- Lugha ya Ekegusii Archived 10 Mei 2007 at the Wayback Machine.