Kukimbilia Misri
Kukimbilia Misri ni tukio linalosimuliwa katika Injili ya Mathayo (2:13-23) halafu katika Apokrifa. Pia lilichorwa mara nyingi na wasanii mbalimbali.
Habari katika Injili ya Mathayo
hariri2:13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; 15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema,
Kutoka Misri nalimwita mwanangu.
16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi. 17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,
18 Sauti ilisikiwa Rama,
Kilio, na maombolezo mengi,
Raheli akiwalilia watoto wake,
Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.
19 Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. 21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. 22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, 23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.
Tanbihi
haririMarejeo
hariri- Albright, W.F. and C.S. Mann. "Matthew." The Anchor Bible Series. New York: Doubleday & Company, 1971.
- Brown, Raymond E. The Birth of the Messiah: A Commentary on the Infancy Narratives in Matthew and Luke. New York: Doubleday; London: G. Chapman, 1977. Updated ed. 1993.
- Clarke, Howard W. The Gospel of Matthew and its Readers: A Historical Introduction to the First Gospel. Bloomington: Indiana University Press, 2003.
- France, R.T. The Gospel According to Matthew: an Introduction and Commentary. Leicester: Inter-Varsity, 1985.
- France, R.T. "The Formula Quotations of Matthew 2 and the Problem of Communications." New Testament Studies. Vol. 27, 1981.
- Gabra, Gawdat (ed.). Be Thou There: The Holy Family's Journey in Egypt. Cairo and New York: The American University in Cairo Press, 2001.
- Goulder, M.D. Midrash and Lection in Matthew. London: SPCK, 1974.
- Gundry, Robert H. Matthew a Commentary on his Literary and Theological Art. Grand Rapids: William B. Eerdmans Publishing Company, 1982.
- Jones, Alexander. The Gospel According to St. Matthew. London: Geoffrey Chapman, 1965.
- Schweizer, Eduard. The Good News According to Matthew. Atlanta: John Knox Press, 1975
Viungo vya nje
hariri- Further reading on the Flight into Egypt in art
- John Calvin's commentary on Matthew 2:19
- Orthodox Wiki article on the Flight into Egypt Includes map, info and links to various articles and videos on the subject.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kukimbilia Misri kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |