Luka Kirby (Uingereza Kaskazini, 1549 hivi; Tyburn, London, 30 Mei 1582) alikuwa Mkristo msomi wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki huko Leuven, Ubelgiji na seminari ya Douai, Ufaransa mwaka 1576.

Alipewa daraja ya upadri huko Cambrai (1577) akaondoka kurudi Uingereza tarehe 3 Mei 1578, lakini mwaka huohuo alikwenda Roma, Italia, alipohudumia Waingereza wenzake wenye shida[1].

Alirudi kwao lakini alipofika tu pwani alikamatwa mnano Juni 1580 kwa uhaini dhidi ya malkia Elizabeti I kwa sababu ya Ukatoliki wake[2]. Aliteswa kikatili na tarehe 17 Novemba 1581 alipewa adhabu ya kifo[3][4].

Aliuawa pamoja na mapadri Williamu Filby na Laurenti Richardson. Wote watatu walitangazwa wenye heri na Papa Leo XIII mwaka 1885. Pamoja nao aliuawa Mjesuiti Thomas Cottam.

Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[5].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[6].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.