Makari Mkuu
Makari Mkuu (300 hivi - 391) alikuwa mkaapweke na padri wa Misri.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Januari, 19 Januari[1] na 4 Aprili kadiri ya madhehebu.
Maisha
haririMzaliwa wa Misri Kusini, aliwahi kufanya biashara ya chumvi, akaoa, lakini mke wake akafa mapema.
Mwaka 330 hivi akawa mfuasi wa Antoni Mkuu jangwani.
Huko alikataa upadrisho akahamia pengine aliposingiziwa vibaya.
Hapo alihamia kwenye jumuia ya bonde la Sketes (leo Wadi El Natrun) alipokubali kupewa upadri na kuwa kiongozi wa kiroho wa wamonaki. Kati ya wanafunzi wake wa miaka 356-384 kuna Sisoe, Isaya, Aio, Mose Mwethiopia, Pafnusi, Zakaria, Teodoro wa Ferme.
Hivyo monasteri yake ilichangia sana ustawi wa umonaki ikadumu hai hadi leo.
Miaka 373-375 askofu Mwario Lusio wa Aleksandria alimpeleka uhamishoni kwa imani yake.
Kama alivyowafundisha wengine, aliishi kwa Mungu tu katika sala, akajulikana kwa hekima yake.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo kwa Kiswahili
hariri- Misemo ya Mababa wa Jangwani (Apophthegmata Patrum) – tafsiri ya W. Ngowi, O.F.M.Cap. – ed. Salvatorianum – Morogoro 2000 – ISBN 0-264-66350-0
Marejeo mengine
hariri- Maloney, GA, SJ (trans.), 1992, Pseudo-Macarius. The Fifty Spiritual Homilies and the Great Letter, CWS, New York: Paulist Press
- Mason, AJ (trans.), 1921, Fifty Spiritual Homilies of St Macarius the Egyptian, London: SPCK
- Plested, Marcus, 2004. The Macarian Legacy: The Place of Macarius-Symeon in the Eastern Christian Tradition. Oxford: OUP
Viungo vya nje
hariri- Spiritual Homilies 1-5 Ilihifadhiwa 28 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine., 6-11 Ilihifadhiwa 28 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine., 12-22 Ilihifadhiwa 28 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Macarius the Great Select Resources, Bilingual Anthology
- Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge, 1914: "Macarius the Egyptian"
- Wesley Center Online [1] Ilihifadhiwa 2 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
- Volume 38, Wesleyan Theological Journal, Academic Article on Macarius of Egypt, pp. 103 – 123 [2] Ilihifadhiwa 29 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.
- Greek Opera Omnia by Migne Patrologia Graeca with Analytical Indexes
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |