Makemake (alama: 🝼;[1] tamka kama ni Kiswahili; jina rasmi: 136472 Makemake) ni sayari kibete inayozunguka jua letu katika umbali mkubwa kwenye ukanda wa Kuiper.

Makemake na mwezi wake.

Iligunduliwa na wanaastronomia Michael E. Brown, Chad Trujillo na David Rabinowitz kwenye paoneaanga pa Mount Palomar tarehe 31 Machi 2005.

Jina

Jina lilichaguliwa kutokana na mungu muumbaji aliyeitwa "Makemake" katika dini asilia ya Kisiwa cha Pasaka (Easter Island, kwenye Bahari ya Pasifiki). Kuna mapatano katika Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kutumia majina ya miungu ya dini mbalimbali kwa magimba yanayoendelea kugunduliwa katika ukanda wa Kuiper. Asili ya jina iko katika lugha ya Kipolinesia na katika dini yao ni muumbaji wa binadamu na mungu wa rutuba. Makemake aliabudiwa kwa umbo la ndege wa bahari. Ishara yake ilikuwa mwanamume mwenye kichwa cha ndege.[2]

Muundo na tabia

Hakuna habari nyingi za uhakika kutokana na umbali wa gimba hili na kwa sababu hadi sasa hakuna chombo cha angani kilichopita karibu nayo. Lakini Makemake inaonekana ni hasa mwamba na barafu ilhali katika baridi iliyopo mbali na jua barafu huwa ngumu kama mwamba.

Marejeo

  1. JPL/NASA (2015-04-22). "What is a Dwarf Planet?". Jet Propulsion Laboratory. Iliwekwa mnamo 2022-01-19. 
  2. Fourth dwarf planet named Makemake, tovuti ya Ukia, 19 Julai 2008, iliangaliwa Julai 2017

Viungo vya Nje

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makemake kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.