Matamasha Makuu ya Afrika Mashariki

Matamasha Makuu ya Afrika Mashariki kati ya mengine mengi yanayovuta watu kutoka mahali pengine ni pamoja na haya yafuatayo.

Mombasa Carnival hariri

Mombasa Carnival ni tamasha lifanyikalo katika mji wa Mombasa, nchini Kenya, ambalo huonyesha historia, utamaduni, na muziki vya Mombasa na nchi ya Kenya kwa jumla. Mombasa ni mji wa pwani, wa pili kwa ukubwa ndani ya Kenya na ina historia kubwa sana.

Tamasha hilo huanza tarehe 1 Novemba na humalizika tarehe 30 Novemba. Wizara ya Utalii huandaa tamasha hilo na linakuwa tamasha kubwa zaidi katika Kenya. Watu kutoka maeneo mbalimbali - Waajemi, Wachina, Waarabu, Wareno, Wahindi, Wazungu na Waafrika kwa jumla - wanafika na kuvutiwa na utamaduni wa Mombasa wa tangu karne ya 12. Wakati wa tamasha hilo kuna kusherehekea katika barabara za Mombasa. Kila jamii ina sehemu ya gwaride na kucheza muziki na kucheza na kuvaa nguo mbalimbali. Unaweza kusikiliza muziki wa aina nyingi kutoka taarab mpaka Afropop na muziki wa kidini. Kabla ya tamasha humalizika wao huungana katika barabara ya Moi na huenda baharini ili kutazama mbio za maboti.

Ziwa la Nyota hariri

Ziwa la Nyota ni tamasha linalodumu siku tatu katika Ziwa Malawi, ambalo ni ziwa la tatu kwa ukubwa zaidi katika Afrika yote. Tamasha hilo lilianza mwaka 2004 na watu hufika kwa maelfu. Tamasha hilo lilianzishwa na mtalii wa Uingereza Will Jameson aliyetembelea Malawi mwaka 1998. Yeye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha John Moores na alichukua likizo ya mwaka mzima ili kuweza kufanya kazi na Jumuiya ya Wanyamapori. Baada ya kurudi chuoni, Jameson alianzisha klabu ya usiku. Klabu hiyo iliitwa Chibuku Shake Shake, jina la chapa ya bia ya Malawi. Mwaka huo Jameson alifanya tamasha la kwanza. Tamasha la Ziwa la Nyota la mwaka 2011 lilivutia zaidi ya wahudhuriaji 3,000 kutoka Ulaya na Afrika. Watu waliokuja miaka iliyofuata katika Ziwa la Nyota wanaweza kusikiliza wazungumzaji, kucheza, kutazama onyesho katika ukumbi wa michezo, kusikiliza muziki au kufanya shughuli za furaha zaidi. Tamasha hilo huanza tarehe 25 Novemba na hufanyika kila mwaka. Watu wengi wanasema tamasha hilo ni moja ya matamasha makubwa zaidi katika Afrika.

Tamasha la Kimataifa la Filamu hariri

Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar au ZIFF ni tamasha ambalo hufanyika mjini Zanzibar katika nchi ya Tanzania. Tamasha hilo hutokea kila mwaka tangu 1997. Lilitengenezwa ili kukuza filamu na sekta nyingine za kitamaduni. ZIFF huonyesha filamu nyingi katika Mji Mkongwe na vitongoji mbalimbali vya kisiwa cha Zanzibar. ZIFF huchukua siku kumi na kuna matukio ya aina nyingi sana. ZIFF kuleta pamoja zaidi ya watu 100,000 kutoka mahali mbalimbali pa ulimwengu. ZIFF kutoa tunzo ya kimataifa kumi na mbili za aina mbalimbali kama Dhow ya Fedha, Maandishi, Filamu fupi, uhuishaji, Talanta ya Afrika Mashariki, Tunzo ya UNICEF na tunzo nyingi zaidi.   

MTN Nyege Nyege hariri

Tamasha la Nyege Nyege ni tamasha katika mji wa Kampala, nchi ya Uganda. Nyege Nyege ni jina la kikundi ambacho kimeanzisha tamasha hilo. Tamasha la Nyege Nyege lilianzishwa mwaka 2015 na hutokea kila mwaka tangu wakati huo. Nyege Nyege kulikuwa na mfadhili anayeitwa MTN, hivyo tangu mwaka 2017 linaitwa MTN Nyege Nyege. Zaidi ya watu 9,000 huenda kusikiliza muziki, kwa hiyo Nyege Nyege ni tamasha la muziki elektroniki kubwa zaidi katika Afrika Mashariki. Nyege Nyege huonyesha hasa wanamuziki kutoka Afrika Mashariki lakini kuna wanamuziki kutoka mahali pengine katika ulimwengu.

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matamasha Makuu ya Afrika Mashariki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.