Metorolojia
Metorolojia (kutoka Kigiriki μετεωρολογία, meteorologia; kwa Kiingereza meteorology) ni sayansi inayoshughulikia habari za angahewa, tabianchi na halihewa na hasa fizikia pamoja na kemia husika.
Tabia za angahewa
haririTabia za msingi za halihewa ni mwendo wa upepo, halijoto, umawingu, unyevu, kanieneo, kiwango cha mnururisho wa jua, uvukizaji na nyingine. Tangu karne nyingi wataalamu wamejitahidi kupima tabia mbalimbali za halihewa na angahewa kama msaada wa kuzielewa vizuri zaidi na kujenga msingi kwa utabiri wake.
Vifaa vya metorolojia
haririMetorolojia imeanza kutokea kadiri wataalamu walivyoanza kuchukua vipimo halisi vya tabia za angahewa na kuvilinganisha. Mwelekeo huo ulileta kubuniwa kwa vifaa vya upimaji maalumu vinavyounganishwa kwenye vituo vya metorolojia. Data kutoka vifaa hivyo zinatunzwa kwa muda mrefu, zinaruhusu kutabiri halihewa na kuangalia mabadiliko ya tabianchi.
- vyombo vya kupimia kiasi cha usimbishaji, hasa mvua, vilivyosanifishwa na serikali vinajulikana kutoka Korea mnamo 1441; vilisambazwa kama msaada wa kukadiria kodi za wakulima. Hadi leo kiasi cha mvua kinachonyesha kwa mwezi au mwaka ni kipimo muhimu kwa kupanga shughuli za kilimo.
- vyombo vya kupimia kasi na mwelekeo wa upepo mahali fulani vinajulikana tangu anemomita iliyobuniwa Italia mnamo 1450. Habari hizo ni za msingi kwa kuelewa uhusiano kati ya hali ya hewa katima maeneo jirani; ni pia muhimu kwa kupanga kilimo kwa sababu zinatawala sehemu ya uvukizaji na ni habari za lazima kwa mpangilio wa usafiri kwa eropleni na pia meli.
- Vipimajoto vilivyofanana na vile vya kisasa vilipatikana tangu karne ya 17 na mwaka 1724 Daniel Gabriel Fahrenheit alianzsha skeli ya kwanza iliyoruhusu kulinganishwa kwa vipimo vya joto.
- Higromita ni kifaa cha kupimia kiwango cha unyevu katika hewa; chombo hicho kilibuniwa mwaka 1783 na Mfaransa Horace-Bénédict de Saussure.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Metorolojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |