Metodi I wa Konstantinopoli

Metodi I wa Konstantinopoli (Siracusa, leo nchini Italia, 788 hivi – Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 14 Juni 847) alikuwa mmonaki na mwandishi wa Kikristo wa Dola la Bizanti.

Picha takatifu ya ushindi wa imani sahihi. Metodi amechorwa upande wa juu kulia.

Alifungwa gerezani kwa sababu ya kutetea matumizi ya picha takatifu[1], lakini hatimaye akawa Patriarki wa Konstantinopoli tangu 4 Machi 843 hadi kifo chake.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Juni[2].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.