Nuru (kutoka Kiarabu نور, nur; pia mwanga) ni neno la kutaja mnururisho unaoweza kutambuliwa kwa macho yetu. Kwa lugha ya fizikia ni sehemu ya mawimbi ya sumakuumeme yanayoweza kutambuliwa na jicho.

Nuru ya jua linaangaza wingu angani

Mawimbi ya nuru huwa na masafa ya nanomita 380 hadi 780 au yenye marudio ya takriban terahezi 789 hadi 384.

Chanzo cha nuru duniani ni hasa jua. Nuru ya jua inaleta pia nishati inayotumiwa na mimea ambayo kwa njia ya usanisinuru inajenga kwa ndani sukari au wanga ambavyo ni lishe za viumbehai vyote vinavyozila. Hivyo nuru ya jua, kwa njia ya usanisinuru, ni chanzo cha nishati kwa karibu viumbehai vyote duniani.

Chanzo kingine cha nuru kwa binadamu ni moto. Lakini hadi karne ya 19 nuru hii ilitumia pia nishati ya jua iliyotunzwa na mimea kwa njia ya kuni, mafuta ya petroliamu au gesi asilia. Ni tangu kugunduliwa kwa umeme tu ya kwamba chanzo tofauti cha nuru kimepatikana.

Nuru kama mnururisho

hariri

Nuru inayoonekana kwetu ni sehemu ya mnururisho wa sumakuumeme. Nuru inayoonekana ni sehemu ndogo tu ya spektra ya sumakuumeme.

 
Nuru inayoonekana kwa macho ni sehemu tu ya mnururisho wa sumakuumeme. Mawimbi ya nuru ni sehemu ya mawimbi mengine ya sumakuumeme

Wanyama wanaweza kuona mawimbi marefu zaidi, yaani infraredi, au mafupi zaidi, yaani urujuanimno.

Aina nyingine za mnururisho huohuo ni kwa mfano joto, eksirei, microwave, mawimbi ya redio ambazo zinatofautiana na nuru kwa idadi ya marudio yake na hazitambuliwi kwa macho au milango ya fahamu, isipokuwa joto linalotambuliwa na ngozi yetu.

Tabia za nuru

hariri

Kati ya tabia za nuru zinazoweza kutofautishwa ni ukali wake, mwelekeo wake, marudio yake.

Kasi ya nuru haibadiliki: ni daima mita 299,792,458 kwa nukta katika ombwe.

Rangi ya nuru inategemea marudio yake.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nuru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.