Mizengo Kayanza Peter Pinda

(Elekezwa kutoka Mizengo Pinda)

Mizengo Kayanza Peter Pinda (amezaliwa 12 Agosti 1948) ni mwanasiasa nchini Tanzania.

Mizengo Pinda alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya Edward Lowassa kujiuzulu.

Alikuwa mbunge tangu mwaka 2000 hadi 2015 na kuwa Waziri Mkuu wa nchi tangu Februari 2008 hadi 2015 alipostaafu siasa.

Maisha

hariri

Pinda alizaliwa Mpanda vijijini katika mkoa wa Rukwa. Yeye ni mtoto wa kwanza wa mkulima maskini.

Alifuata elimu hadi kutunukiwa shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1974.

Mwaka uleule akajiunga na utumishi wa serikali kama wakili wa serikali katika Wizara ya Katiba na Sheria.

Mwaka 1978 akahamia ofisi ya Usalama wa Raia kwenye Ikulu ya rais, kwanza chini ya Julius Nyerere, halafu chini ya Ali Hassan Mwinyi.

Kuanzia mwaka 1982 akaendelea kuwa Katibu Mnyeka Msaidizi wa Rais hadi mwaka 1992.

Tangu mwaka 1996 hadi 2000 akawa Katibu wa Baraza la Mawaziri.

Bungeni ameingia mwaka 2000 kama mbunge wa Mpanda Mashariki mkoani Rukwa akawa naibu waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa tawala za mikoa na serikali za mitaa.

Mwaka 2006 akapandishwa cheo kuwa waziri kamili.

Baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Pinda aliteuliwa na rais Jakaya Kikwete na kuthibitishwa na bunge kwa kura 279 za ndio katika jumla ya kura 283 zilizopigwa.

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 aliendelea na wadhifa huo. Mwaka 2015, alikuwa ni mmoja kati ya makada 38 wa Chama Cha Mapinduzi ambao walichukua fomu kuomba kukiwakilisha chama chake katika kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu uliotarajiwa kufanyika nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka 2015. Pinda alikuwa ni mmoja wa vigogo walioondolewa kwenye mchakato huo katika hatua za awali.

Viungo vya nje

hariri


  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mizengo Kayanza Peter Pinda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.