Njombe (mji)
Njombe ni halmashauri ya mji wenye hadhi ya wilaya ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Njombe, nchini Tanzania, yenye postikodi namba 59100. Kabla ya kugawiwa eneo la Njombe lilikuwa sehemu ya Mkoa wa Iringa.
Njombe | |
Mahali pa mji wa Njombe katika Tanzania |
|
Majiranukta: 9°20′00″S 34°46′00″E / 9.33333°S 34.76667°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mkoa wa Njombe |
Wilaya | Wilaya ya Njombe Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 182,127 katika eneo la halmashauri |
Misimbo ya posta ni 59101 (mjini, CBD) hadi 59117.
Njombe iko kwenye kimo cha mita 2,000 juu ya UB kwenye sehemu ya mashariki ya milima ya Kipengere, hivyo tabianchi ni baridi kiasi[1].
Mji uko takriban kilomita 200 kusini kwa Iringa na kilomita 150 upande wa kaskazini-mashariki kwa Mbeya.
Hadi mwaka 2012 kata za mji wa Njombe zilikuwa sehemu ya Wilaya ya Njombe ya awali; baadaye Njombe Mjini na Wilaya ya Njombe Vijijini zilitengwa kuwa halmashauri mbili za pekee.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 182,127 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ya Njombe Mjini ilikuwa na wakazi wapatao 130,223 waishio humo. [3]
Wenyeji ni hasa Wabena. Lakini pia, kuna wingi wa watu wa makabila mengine kama Wakinga na Wapangwa.
Usafiri
haririBarabara ya lami kutoka Makambako kwenda Songea inapita mjini. [4]
Kituo cha karibu cha treni za TAZARA kipo Makambako. Pia kuna uwanja wa ndege eneo la Chaugingi.
Hakuna huduma ya ndege za abiria.
Dini
haririNjombe ni makao makuu ya Dayosisi ya Kusini KKKT ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na pia ya Jimbo Katoliki la Njombe ya Kanisa Katoliki Tanzania. Kuna pia makanisa mengine na misikiti.
Eneo la Yakobi katika mji wa Njombe linatunza jina la kituo cha Wamisionari Walutheri Wajerumani waliofika mnamo mwaka 1899. Wakati wa Vita ya Majimaji kituo cha Yakobi kilishambuliwa na kikosi kilichoongozwa na chifu Mbeyela.[5]
Marejeo
hariri- ↑ Tanzania travel guide (toleo la 6). Lonely Planet. Juni 2015. uk. 271. ISBN 978-1742207797. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2016.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Sensa ya 2012, Njombe Region – Njombe Town-Council
- ↑ "Njombe Roads Network" (PDF). Tanroads. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-05-10. Iliwekwa mnamo 14 Februari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Seth I Nyagava, "Were the Bena traitors? Majimaji in Njombe..", mlango wa 7 katika "Maji Maji: Lifting the Fog of War", James Leonard Giblin, Jamie Monson BRILL, 2010; hapa uk. 247
Kata za Wilaya ya Njombe Mjini - Tanzania | ||
---|---|---|
Ihanga | Iwungilo | Kifanya | Lugenge | Luponde | Makowo | Matola | Mjimwema | Njombe Mjini | Ramadhani | Utalingoro | Uwemba | Yakobi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Njombe (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |