Mkoa wa Mashariki (Kenya)
| ||
Makao Makuu | Embu | |
’‘‘Mji Mkubwa’’’ | Machakos | |
Eneo - Jumla |
Nafasi ya 2 kati ya mikoa ya Kenya 154,354 km² | |
Wakazi - Jumla (2007) - Msongamano wa watu / km² |
Nafasi ya 2 kati ya mikoa ya Kenya 5,380,200 35/km² | |
Lugha mkoani | Kikamba, Kimeru lugha za wahamiaji kama Kiturkana Kiborana | |
Mkoa wa Mashariki (Eastern Province) ni mkubwa wa pili kati ya mikoa minane ya Kenya. Umepakana na Ethiopia halafu na mikoa ya Bonde la Ufa, Kati, Nairobi, Pwani na Mashariki-Kaskazini.
Eneo la mkoa ni 154,354 km² kuna wakazi karibu milioni tano na nusu. Umbo lake ni kanda ndefu linalounganisha watu wenye maisha na utamaduni tofauti sana. Katika kusini kuna wakulima wanaotumia lugha za Kibantu kama vile Wakamba na Wameru. Maeneo mapana ya kaskazini ni yabisi yakikaliwa na wahamiaji kama Borana, Turkana, Wasomali na wengine. Makao makuu ya mkoa yapo mjini Embu.
Ndani ya mkoa kuna maeneo yenye rutba sana hasa karibu na Mlima Kenya. Sehemu kubwa za Ukambani ni yabisi kiasi na wakulima wake hukosa mvua kila baada ya miaka kadhaa na kuteswa na njaa. Kaskazini ni nchi yabisi hata jangwa kama jangwa la Chalbi kati ya Ziwa Turkana na Marsabit.
Wilaya
hariri- Wilaya - (Makao Makuu)
- Embu - (Embu)
- Isiolo - (Isiolo)
- Kitui - (Kitui)
- Machakos - (Machakos)
- Makueni - (Wote)
- Marsabit - (Marsabit)
- Mbeere - (Siakago)
- Meru Central - (Meru)
- Meru North a - (Maua)
- Meru South b - (Chuka)
- Moyale - (Moyale)
- Mwingi - (Mwingi)
- Tharaka - (Tharaka)
a Inaitwa piaWilaya ya Nyambene.
b Inaitwa pia Wilaya ya Nithi.
Bonde la Ufa | Kaskazini-Mashariki | Kati | Magharibi | Mashariki | Nairobi | Nyanza | Pwani |